WAZIRI
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imevitaka vyama ambavyo
wachezaji wake waliiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki
kuwasilisha ripoti kuanzia jinsi walivyojiandaa, kushiriki hadi matokeo
waliyopata.
Agizo
hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Leonard
Thadeo, katika hafla ya kuikaribisha timu ya Olimpiki ya Tanzania na
kurejesha bendera ya taifa serikalini.
Akitoa
maagizo hayo ya Waziri, Dk. Fenella Mukangara, Mkurugenzi huyo alisema
waziri ameagiza viongozi wa vyama hivyo na vile vilivyokuwa katika
mpango wa kusaka viwango vya kushiriki michezo hiyo, waandae tathmini ya
ushiriki wao kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuiwakilisha
kwake.
“Viongozi
wa vyama muandae tathmini ya ushiriki wenu wa Olimpiki, nini kimetokea
ndani ya miaka minne, mlifanya nini, mlikwama wapi na nini kifanyike,”
alisisitiza Thadeo kwa niaba ya waziri, ambaye alikuwa akihudhuria vikao
vya Bunge mjini Dodoma na kuongeza:
“Kama
mlivyosema, maandalizi yanatakiwa yaanze kesho, sasa ili twende Brazil
2016 lazima tuwe tumejipanga kwa kutambua tatizo, kwa kufanya tahmini na
kuweka mipango ya pamoja, ikiwashirikisha washika dau mbalimbali, si
kwamba tunataka twende Brazil wakati vikwazo bado vipo palepale.”
Pia
Mkurugenzi huyo aliwasilisha salamu za pongezi kwa wanamichezo hao,
kwani kushiriki kwao kulitokana na kufuzu vigezo na wala si kupendeleana
wala urafiki, hivyo wamejitahidi kwa kadiri ya uwezo wao, hivyo
wakaribie nyumbani.
“Mheshimiwa
Waziri, anawakaribisheni na kuwapongeza sana, mmekutana na mengi sana
ya ‘kuwa- discourage’ lakini mmepambana, mengi yametokea, hamkwenda huko
kwa utashi wa mtu, mmepita katika vigezo, ni jambo la kujivunia,
mmevipita vigezo na si urafiki, tuchukulie kama chachu, tukifanya vizuri
tutapongezwa tu,” alisema.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Rais wa TOC, Ghulam Rashid, alisema matokeo
hayo yametokana na aina ya maandalizi yaliyofanywa na vyama kwa
kushirikiana na Kamati ya Olimpiki (TOC), huku akiwataka Watanzania
kutambua kwamba ili kupata mafanikio katika mashindano ya kimataifa,
inahitajika maandalizi na vifaa vya uhakika, vitu ambavyo viko juu ya
uwezo wao, hivyo kila Mtanzania anatakiwa kusaidia kwa hali na mali.
“Tunaomba
Watanzania waelewe, ili mchezaji afanye vizuri inahitajika maandalizi
ya uhakika na ya muda mrefu na vyama vyetu ni malofa, haviwezi pekee
yao, hivyo tunawajibu wa kuvisaidia ili viweze kuwaandaa vema na
hatimaye kuja kufanya vema,” alisema Ghulam.
Katika
Olimpiki London 2012, Tanzania iliwakilishwa na wanariadha, Samson
Ramadhani ambaye alikuwa nahodha, Faustine Mussa, Zakia Mohamed na
Msenduki Mohamed, ambaye hata hivyo hakukimbia baada ya kushikwa na
nimonia, bondia Selemani Kidunda, waogeleaji Magdalena Moshi na Amaar
Ghadhiar.Chanzo:http://francisdande.blogspot.com/2012/08/waziri-mukangara-ataka-ripoti-ya.html
Post a Comment