Kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Bara
itaandika historia msimu ujao, ambapo sasa itasimamiwa na kuendeshwa na
kampuni, 'Tanzania Premium League' (TPL). Hatua ya kupitisha mabadiliko
hayo, ilifikiwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati ya kuendesha mchakato wa kampuni, Wallace Karia alisema TFF imepitisha kampuni kuwa chombo huru cha kuendesha ligi hiyo itakayoanza rasmi Septemba Mosi mwaka huu."Tulichokuwa tunatofautiana na TFF juu ya ligi kuendeshwa na chombo huru, lakini sasa kamati ya utendaji imetoa baraka," alisema Karia."Kuna mambo madogo ya kufanyiwa mabadiliko, hata hivyo hali hiyo siyo kikwazo cha ligi kusimamiwa na chombo huru," aliongeza Kiria.Karia alisema baadhi ya maeneo ya kufanyiwa marekebisho ni suala la muundo wa kisheria wa uendeshaji ligi na kasoro ndogo walizozibaini awali.
Kimuundo kutakuwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa TPL, kiongozi wa juu wa klabu iliyoshinda Ligi Kuu msimu uliotangulia.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Post a Comment