WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe: Samuel Sitta amezidi kulia na
ufisadi, rushwa na wizi unaoendelea kuangamiza uchumi wa taifa.Sitta
ambaye pia alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, amesema kuwa mtandao wa wala
rushwa nchini ni mkubwa na watu wachache wameupenyeza katika Serikali,
CCM na sasa umeanza kulitikisa hata Bunge.
Waziri Sitta alisema
hayo juzi baada ya kupokewa na wakazi wa Mji wa Bukoba alipowasili
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabiani Massawe,
kwa ajili ya ziara ya siku tano ya kikazi.Wakazi wa mji huo
walimpokea kwa kumuimbia nyimbo zikiwemo za mapambano dhidi ya rushwa na
ufisadi wakilalamika mafisadi wanatakata kuneemesha matumbo yao na
familia zao, huku wakiwaacha wananchi wengi wakinyong'onyea.
Chanzo kwa hisani ya http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/25806-sitta-alia-na-ufisadi-ccm-bungeni
Post a Comment