Mgeni rasmi Mh: Said Mecky Sadick Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akikabidhi kombe kwa nahodha wa Yanga Nadir Haroub Canavaro |
Shukrani
kwao Hamisi Kiiza Diego na Said Bahanuzi, wafungaji wa mabao hayo moja
kila kipindi na sasa Yanga inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager,
inaingia kwenye orodha ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, kwa
kutwaa taji hilo mara tano.
Yanga
sasa imebakiza mara moja kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi,
Simba (1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002) kutwaa Kombe hilo, mara
tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.
Kiiza
alifunga bao lake, baada ya kuuwahi mpira aliokuwa anarudishiwa kipa
Deo Munishi ‘Dida’ na beki Said Mourad na kumpiga chenga kipa huyo kisha
kuusukuma mpira nyavuni.
Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya kumtungua Dida.
Mechi
hiyo ilichezeshwa vema na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi,
aliyekuwa akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa
Kenya.
Katika
mchezo huo kikosi kilichoweka historia ya Kombe la tano la Kagame,
Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar
Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’,
Rashid Gumbo/Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi
Kiiza na David Luhende.
Azam
FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad,
Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche/Mrisho Ngassa, Salum Abubakar,
John Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo,
Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.
Katika
mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao
yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika
ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa
na Jean Mugiraneza dakika ya 89.
Post a Comment