SERIKALI imesema kuwa hakuna malipo ya kiasi kidogo cha fedha
kilicholipwa kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu ya Kambi ya jeshi
ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 kama ilivyoripotiwa na gazeti moja
la kila wiki la hapa nchini hivi karibuni.
Akizungumza na Idara ya Habari( MAELEZO) jana ofisi kwake , Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema hakuna fidia ya Shs.
1400 na Shs. 2500 iliyotolewa kuwa ni ya uharibifu wa jumla ya fidia za
malipo kwa wahanga hao, bali malipo hayo ni tofauti ya kiasi cha fedha
kilichokuwa kinadaiwa na wahanga hao ambacho kilichobakia.
‘’ Unajua malipo ya wahanga hao yalifanyika katika awamu mbili. Hivyo
kiasi cha fedha cha malipo hayo yaliyotolewa katika hundi hizo ,
ambayo iliripotiwa katika gazeti hilo ni malipo ya awamu ya tatu.
Malipo hayo ni tofauti ya fedha kilichokuwa kinadaiwa na si kweli
kuwa wahanga hao walilipwa fedha hizo kama jumla ya fidia za malipo
yao,’’ alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa, aliongeza kuwa habari hiyo iliyoandikwa sio sahihi
na haikufuata maadili ya uandishi wa habari kwani hakuweka wazi usahihi
wa taarifa hiyo.Serikali haijamdhulumu mtu yeyote, bali inalipa kutokana
malipo stahili.
‘’Ninaomba waandishi wa habari waandike habari walizozifanyika utafiti
wa kina wa pande zote ilikuepusha utoaji wa taarifa zisizosahihi,’’
alisisitiza.
Aidha Mkuu huyo alisema malipo ya waathirika hao yanatolewa kwa awamu
tofauti na kwa idadi ya watu maalum, kwa sababu ya kuepusha utoaji wa
malipo yasiyostahili. Hivyo aliwataka waathirika hao kuvuta subira kwa
kuwa malipo hayo bado yanaendelea.
Naye Mtathimini Mkuu wa malipo hayo, Victor Ndonne akizungumzia kuhusu
suala hilo alisema hundi za malipo ya sh. 1000 na zilizotajwa hapo juu
ni za tofauti ya kiasi cha fedha kilichobakia baada ya wahanga hao
kutoridhika na malipo hayo yaliyotolewa katika awamu ya kwanza na awamu
ya pili.
Chanzo; Full Shangwe Blog
Post a Comment