Social Icons

Loading...

Kisa cha Mchungaji wa kanisa na Mmasai

Kuna kisa cha Mchungaji wa Kanisa la Kibabtisti aliyefika kijiji cha Wamasai Jumapili moja kuhubiri dini. Mchungaji akawa na nia  pia ya kuanzisha kanisa kijijini hapo.

Wamasai wakakusanyika kanisani. Baada ya kuhubiri Neno la Mungu kwa saa mbili, Mchungaji akaomba arudi tena kijijini hapo Jumapili  inayofuata. 

Ndipo hapo akasimama Mzee wa Kimasai na kutamka;

Mzee wa Kimasai; " E bwana Chungaji sisi iko furahia sana neno yako ya Mungu. Lakini, usije juma la kesho, ni kwa vile kuna ile padri ya Roman imesema inakuja kusema neno ya Mungu pia."

Mchungaji: " Je, inawezekana nikaja Jumapili ya keshokutwa?"

Mzee wa Kimasai: " Hapana, Chungaji, Jumapili ya keshokutwa kuna ile Imam ya Msikiti  imesema inakuja kutupa mawaidha ya Kiislamu"

Mchungaji: " Sasa nyinyi hamuwezi kuchanganya  dini na madhehebu, itabidi mchague!"

Mzee wa Kimasai: " Aisee Baba Chungaji, wewe iko chungaji na mimi pia ni chungaji. Zile ng'ombe nachunga zinakula majani pamoja. Wake zetu zinashinda na kufanya kasi pamoja. Watoto zetu sinacheza pamoja. Sasa sisi hatutaki hiyo dini inakuja kutagawa hapa".
 source:  Mjengwa blog
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top