Presha, pupa za kocha Zradvok Logarusic pamoja na kujiamini
kupita kiasi kwa wachezaji na kukosa mipango katika safu kiungo na
ushambuliaji vilichangia kuiua Simba.
Simba ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KCCA ya Uganda katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika mchezo huo kocha wa Simba Logarusic
alionekana kuchanganyikiwa na kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili
katika dakika 30 za kipindi cha kwanza.
Mcrotia huyo alimtoa beki Haruna Shamte dakika ya
19 za mchezo na kumwingiza William Lucia na dakika 29, alimtoa Awadh
Juma na kumwingiza Ramadhani Chombo.
Pamoja na ujanja wa kocha Loga kujaza viungo wengi
ili kutawala mchezo huo bado Waganda hao walifanikiwa kuharibu mipango
yote ya Simba kwa kucheza soka ya kasi.
Taarifa zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Kilichoiponza-Simba-kwa-KCCA/-/1597534/2146718/-/e5vaye/-/index.html
Taarifa zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Kilichoiponza-Simba-kwa-KCCA/-/1597534/2146718/-/e5vaye/-/index.html
Post a Comment