Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamemsainisha mkataba wa miezi
sita kocha wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, Hans Van der Plujim.
Mholanzi huyo kiboko wa kocha mkuu wa Simba,
Zdravko Logarusic, mwaka 2012 alikiingoza kikosi chake cha Berekum
Chelsea kuitandika Ashanti Gold Field mabao 4-0 iliyokuwa ikifundishwa
na Mcrotia huyo.Uongozi wa Yanga umempa mkataba wa miezi sita
kocha huyo huku ukimpa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja endapo matokeo
yatakuwa mazuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kocha Plujim alisema amekuja kufanya kazi na siyo vinginevyo kwani ana uzoefu wa soka la Afrika.
Alisema kuwa amefundisha soka Ghana na Ethiopia na
anajua mazingira ya timu za Afrika hivyo amekuja Tanzania kuleta
changamoto mpya.
“Nimekuja kufanya kazi na si kitu kingine, najua
Yanga ni timu kubwa, ila wachezaji wanatakiwa kufuata sheria na kuwa na
nidhamu ya hali ya juu, ndani na nje ya uwanja,” alisema Plujim (65).
Alisema kuwa staili yake ya ufundishaji ni kushambulia muda wote na kuweka ulinzi mkali wa kuzuia kufungwa.
soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Logarusic-ampa-ulaji-kocha-Yanga/-/1597534/2145488/-/cx05llz/-/index.html
soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/Michezo/Logarusic-ampa-ulaji-kocha-Yanga/-/1597534/2145488/-/cx05llz/-/index.html
Post a Comment