Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonya kwamba yeyote atakayewasaliti
Wanyarwanda na Serikali yake anastahili kuchukuliwa hatua kali na
kwamba amejitolea maisha yake kuijenga na kuhakikisha Rwanda inakuwa
salama dhidi ya wote wasio na mapenzi mema.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuliombea
taifa juzi, Kagame aliwataka Wanyarwanda wote kuungana katika kusimamia
misingi sahihi na msimamo wao kama taifa, bila kujali tetesi zinazotoka
katika mataifa ya nje kuhusu wale waliotangaza kuisaliti Serikali yake.
Japokuwa hakutaja moja kwa moja kuhusu tuhuma
zinazoikabili Serikali yake kuhusiana na mauaji ya aliyewahi kuwa Mkuu
wake wa Ujasusi aliyeuawa Januari mosi akiwa hotelini huko Afrika
Kusini, Patrick Karegeya, alisema wale wote wanaoigeuka nchi yao na
kuchagua kuua raia wasio na hatia kwa sababu zao binafsi wanastahili
kushughulikiwa ipasavyo.
“Sitakuwa na huruma na watu ambao wanasahau namna
Rwanda ilivyowatengeneza na kuwa hapo walipo na hatimaye wanaamua
kuisaliti kwa kuua raia wa Rwanda wasio na hatia, wakiwemo kinamama na
watoto,” aliongeza.
chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/afrika-mashariki/Kagame--Tutamshughulikia-yeyote-anayeisaliti-Rwanda/-/1597272/2145326/-/h6b3rt/-/index.html
chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/afrika-mashariki/Kagame--Tutamshughulikia-yeyote-anayeisaliti-Rwanda/-/1597272/2145326/-/h6b3rt/-/index.html
Post a Comment