Kampuni ya Vodacom Tanzania na Mwananchi Communications Limited
(MCL), zimezindua mradi wa kufikisha habari za punde (Breaking News) kwa
jamii, kuanzia leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Dar es
Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza alisema kwa
kuanzia, wanatarajia wateja wasiopungua milioni kumi kujiunga na huduma
hiyo.
“Mtumiaji mtandao wa Vodacom ataunganishwa na
huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye neno Habari kwenda namba 15569, kwa
gharama ya Sh150 kwa siku, tunafurahia hatua hii kwani tuna hakika
itatuimarisha sokoni,” alisema Rene.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando alisema mradi huo umegharimu mwaka mmoja na nusu kuuandaa.Mhando alisema mradi huo ni wa kitaifa na
kimataifa, lengo ni kuwawezesha kupata habari yoyote kubwa, duniani na
kuirusha papohapo kwa atakayekuwa amejiunga nao.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/Vodacom--MCL-wazindua-habari-kwa-simu/-/1597570/1878420/-/ryt889z/-/index.html
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/Vodacom--MCL-wazindua-habari-kwa-simu/-/1597570/1878420/-/ryt889z/-/index.html
Post a Comment