Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Kituo cha Televisheni
cha Star, imeingia katika mgogoro na Kampuni ya Ving’amuzi ya Startimes
na kufikia uamuzi wa kuitoa kurusha matangazo ya televisheni ya kituo
hicho.Hatua hiyo ya Kampuni ya Startimes kuondoa Star Tv kwenye orodha ya vituo vinavyopatikana kwenye king’amuzi chake ilianza juzi.
Startimes ilianza kutoa taarifa kuwa kutokana na
matakwa ya Star Tv, wameamua kuitoa kwenye orodha ya chaneli zao bila ya
ufafanuzi wa kina kuhusu uamuzi huo.Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia,
Profesa Makame Mbarawa, alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa kitendo hicho,
alisema hafahamu lolote.
“Sifahamu kwani niko Pemba lakini labda watafute
Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (Mkurugenzi wa
TCRA) watakuwa wanajua,” alisema Profesa Mbarawa.Profesa Nkoma hakupatikana jana na juhudi za
gazeti hili zilifanikiwa kumpata Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent
Mungi aliyesema hafahamu sababu za Startimes kuitoa Star Tv katika
kurusha matangazo ya dijitali.
“Kulikuwa na matatizo ya makubaliano baina ya
pande hizo mbili, Star Tv walilalamika jinsi ya kuonekana kwa chaneli
yao kwa mtoa huduma,” alisema Mungi.
Mungi alisema kwa mujibu wa leseni ya kurusha
matangazo ya kimataifa, Star Tv inatakiwa kuonekana katika dijitali zote
za ndani na uamuzi waliochukua unakiuka makubaliano hayo. “Hata kama
kulikuwa na matatizo, hawakutakiwa kuchukua uamuzi huo, kwani
wangekutana na mamlaka husika (TCRA) na kusikiliza malalamiko hayo kisha
kuwasuluhisha na tatizo hilo likamaliza,” alisema Mungi.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1877332/-/yoj4ag/-/index.html
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1877332/-/yoj4ag/-/index.html
Post a Comment