VIJANA
watatu wa jijini Dar es Salaam, wameibuka washindi katika shindano la Dk.
Reginald Mengi la ‘Kutwit’ kuondoa umasikini nchini.Mshindi wa
kwanza katika shindano hilo lililopewa jina la Twiti Wazo Jipya Kuondoa
Umasikini ni Jilly …. ambaye aliibuka na kitita cha sh milioni moja, Peter
George (sh 500,000) na Ludovick Angelino (300,000).Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika Ofisi za
Makao Makuu ya IPP, Dk. Mengi alisema shindano hilo lina lengo la kuibua mawazo
mapya jinsi ya kupambana na umasikini.
Alisema
washiriki wa shindano hilo lililozinduliwa Mei 13 na washiriki wengi
walijitokeza kuibua mawazo mapya na washiriki watatu ndio walioshinda.Dk. Mengi
ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, alisema mchakato wa kupata
washindi, ulisimamiwa na Kiongozi wa Taasisi ya Chuo cha Uongozi na
Ujasiliamali (IMED), Donath Olomi na jopo lake.
Akizungumza
jinsi washindi hao walivyopatikana, Dk. Olomi alisema jumla ya Twits 481
zimepokelewa kati ya Mei 13 hadi 31.Alisema
vigezo
vilivyotumika katika mchakato huo ni wazo lililoeleweka na kuelezeka
kirahisi, lisiwe wazo ambalo limeshasikika mara nyingi
na liwe linaweza kutekelezeka.
Alisema mshindi wa kwanza Jilly alitoa wazo lililosema ‘Tuwe na utamaduni wa kupenda kile tukifanyacho, tukifanya kwa moyo, uadilif, heshima na kujali muda hata kama it’s self employed.
Taarifa kwa hisani ya blog ya Haki Ngowi.
Post a Comment