Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Dk Charles
Kitima amekitabiria kifo Chama Cha Mapinduzi kama kitaendelea na mtindo
wa kuwanyima fursa wazawa katika maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la kujadili amani na
maendeleo na mpango wa miaka mitano wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini
nchini lililofanyika chuoni hapo jijini Mwanza, Dk Kitima alisema nchi
haiwezi kufikia dira ya maendeleo ikiwa Serikali imeshindwa kutoa
kipaumbele katika utawala mzuri wa rasilimali na wazawa“CCM isipojirekebisha itakufa mapema kama isipoipa
kipaumbele sekta binafsi ya wazawa katika kusimamia rasilimali ya
nchi.Tunataka rasilimali za nchi tusimamie wenyewe,” alisema Charles
Kitima.Akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi katika Ofisi
ya Rais, Uhusiano na Urtatibu, Steven Wassira aliyekuwa mgeni rasmi,
aliongeza kuwa nchi itaendelea kwa kuwapa fursa wananchi wake.
Post a Comment