WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA
UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA
MGENI RASMI MHE. RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE
Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) inawatangazia na kuwaalika wadau na wananchi wote kuhudhuria Warsha
ya Wazi (Open Day) kupata maelezo,
kujadili na kutoa maoni juu ya miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali
kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya kipaumbele
yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16).
Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa
kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa kimaabara (labs)
Huu ni mfumo ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha
ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezeaji wa
miradi ya kipaumbele ya Kitaifa.
Warsha hiyo ya wazi itafanyika ijumaa tarehe 24/05/2013 katika
viwanja vya Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
jijini Dar Es Salaam
kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Wote mnakaribishwa!
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu
DAR ES SALAAM
Post a Comment