Wakati mkutano wa 11 wa Bunge ukiendelea mjini Dodoma, Mbunge wa
Mwibara Kangi Lugola (CCM), ameendelea kuwa mwiba kwa Serikali yake
huku akisema hakuna wa kumnyamazisha kuhusu hoja za kutetea Watanzania,
kwa mambo yasiyofaa.Katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, mbunge
huyo ameeleza ya moyoni kuwa amekuwa akipingana na hoja za Serikali
ikiwamo inayohusu bajeti zake ambazo alisema nyingi zimewekwa
kinadharia.
“Nashukuru kwa kutaka kujua ukweli juu yangu, mara
nyingi watu wamekuwa wakinituhumu mimi na wabunge wengine kuwa
tunaisaliti Serikali na chama chetu, huo ni unafiki maana wanaoisaliti
ni hao wakina ‘ndiyo mzee,’’anaanza kusimulia.Swali. Nini maana yake unaposema wanaoisaliti CCM
ni hao wanaokubali kila kitu, kwani kukubali na kupinga huoni ni tofauti
na kwamba anayepinga ndiye msaliti.
Jibu: Ngoja nikwambie (mwandishi), sisi tunaopinga
baadhi ya bajeti za wizara ndiyo tunaojua uchungu wa chama chetu kwa
sababu tunataka chama kiendelee kubaki madarakani, lakini hao
wanaopitisha pamoja na madudu si wema kwa chama hata siku moja, watakosa
majibu siku ya mwisho.
Akitetea hoja hiyo anaeleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzim imeainisha mambo mengi yanayotakiwa kutekelezwa.Anasema
hata hivyo baadhi ya wabunge wanafanya kila kitu kwa kujipendekeza bila
ya kujua kwamba kupitisha madudu hakufanyi ilani itekelezwe kwa wakati.
Swali. Kwani usipounga mkono ndiyo mambo yanatekelezwa.
Jibu. Ujue kuwa wakati wa uchaguzi mkuu vyama huenda kuomba ridhaa ya wananchi waviunge mkono, jambo hilo linakwenda sambasamba na ahadi zisizotekelezeka, sasa usipokuwa makini na hizo bajeti, unadhani utafanyaje mwisho wa siku kama si kuambulia patupu.
Jibu. Ujue kuwa wakati wa uchaguzi mkuu vyama huenda kuomba ridhaa ya wananchi waviunge mkono, jambo hilo linakwenda sambasamba na ahadi zisizotekelezeka, sasa usipokuwa makini na hizo bajeti, unadhani utafanyaje mwisho wa siku kama si kuambulia patupu.
Anasema bajeti nyingi za Serikali huwa hazitoi
majibu hata kidogo, lakini wabunge wamekuwa wakiogopa kuzikataa kwa
kuhofia kuwa wataambiwa wanapingana na Serikali yao.
Chanzo gazeti la mwananchi.
Post a Comment