Facebook, mitandao mingine ya kijamii pamoja na huduma
ya ‘blackberry mesenger’ maarufu kama BBM huathiri watu kisaikolojia,
husababisha ndoa kuvunjika pamoja na usaliti katika uhusiano,
wanasayansi wamebaini.Utafiti huo uliofanywa mwaka 2012 na wanasayansi
wa nchini Israel umebaini kuwa kwa wastani, wanawake wanatumia dakika 81
katika mitandao ya kijamii kwa siku ukilinganisha na wanaume ambao
hutumia dakika 64, huku watu wasio na elimu wakionekana kuathirika zaidi
na mitandao hiyo.Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv
walihusisha matukio kadhaa ya kisaikolojia kati ya watu walioathirika na
mtandao na udanganyifu uliosababishwa na uhusiano unayoanzishwa kupitia
mitandao ya kijamii.Utafiti huo ulibaini kuwa wote waliohusishwa
walikuwa na tatizo la upweke, ingawa hakuna aliyekuwa na historia ya
matumizi ya dawa za kulevya au matatizo ya kisaikolojia.Watu wenye upweke walionekana kupendelea kutafuta
uhusiano kupitia mitandao, jambo linaloelezwa kusababisha kuwaumiza watu
hao na kuhisi kusalitiwa.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Uri Nitzan kutoka Chuo
Kikuu cha Sackler mchepuo wa Tiba na Afya ya Akili, Shalvata Mental
Health Care Centre alisema: “Kama ilivyo matumizi ya mtandao yanazidi
kuwa makubwa. Vivyo hivyo inavyozidi kuhusiana na masuala ya saikolojia.
Mawasiliano ya kompyuta kama Facebook na makundi ya mawasiliano
yaliyopo ndani ni sehemu muhimu ya habari hii.”
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Facebook--mitandao-ya-kijamii-huathiri-watu-kisaikolojia-/-/1597592/1849998/-/tl3712z/-/index.html
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Facebook--mitandao-ya-kijamii-huathiri-watu-kisaikolojia-/-/1597592/1849998/-/tl3712z/-/index.html
Post a Comment