Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la
tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo
nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza
kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na
sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa
limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni
kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu
isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani
katika nchi yetu,” alisema Pengo.Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli
ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na
ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote
ile.
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu
kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba
waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba
Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile.
Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa
nani,” alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu
haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani
itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli
kama ulivyo,” alisema.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1845566/-/12t0yew/-/index.html
Post a Comment