Wakenya wanapiga kura katika uchaguzi mkuu leo kwa mara
ya kwanza tangu kupitishwa katiba mpya hapo mwaka 2010, inayoingia
katika mfumo wa serikali ya kugawanya madaraka. Kura ya mwaka huu
inajumuisha wagombea 1,882 kwa nafasi za kuchaguliwa, wabunge 290,
maseneta 47, magavana wa majimbo 47, wawakilishi wanawake wa majimbo 47,
kata za uraia 1,450 na nafasi ya uraisi.
Kuna wagombea wanane wa urais, lakini kwa mujibu wa mwenendo wa
kampeni, ushindani mkubwa upo baina ya Raila Odinga (68) wa Muungano wa
CORD na Uhuru Kenyatta (52) wa muungano wa Jubilee. Wagombea wengine wa urais ni Musalia Mudavadi (53) kupitia muungano
uitwao Amani, Martha Karua kupitia muungano wa NARC, Peter Kenneth (48)
wa muungano wa Eagle, Mohamed Abduba Dida (39) wa muungano wa Alliance
For Real Change (ARK), Paul Muite (68) wa Safina na Profesa James ole
Kiyiapi (52) kupitia Restore and Build Kenya.




Post a Comment