NDUGU YANGU MPENDWA,
LEO NINA KISA CHA KWELI KUHUSIANA NA YANAYOJIRI HAPA BONGO LABDA NA MIJI MINGINE.
JUMAPILI ILIYOPITA MJOMBA WANGU ALIKUWA
KWENYE DALADALA AKITOKEA UBUNGO KWENDA
TEGETA. BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE WAKAWA
WAMESIMAMA,KATI
YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA
LAPTOP
HIVI. YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWA KUWA
YEYE
ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA MUMSAIDIA KALE KA BAG" BAADA YA VITUO
VIWILI
YULE JAMAA MWENYE KA BAG ALITEREMKA BILA
MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA
WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.
KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU WALIOJITAMBULISHA
KWAMBA
WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU
ABIRIA
WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO MMOJA WA WALE POLISI, WALIMFUATA
MJOMBA
WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO
LANGU KWA
HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI
TUONESHE"
AKAANGALIA KATI YA WALE ABIRIA WENZAKE HAKUMUONA.
|
CHUNGA SANA KAMA HUYU MZEE YUKO MAKINI HAPA!!! |
WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA SILAHA AINA
YA
PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA KUJIELEZA HUKO.
BASI
LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIA WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA
WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHA KATIKA KESI YA
WIZI WA
KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA MPAKA SASA BADO YUPO
NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE
MAKINI NA
MISAADA TUNAYOITOA. MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA
UMEMGHARIMU MAISHA. Mwisho napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na
watu
tusiowajua,
MTUMIE NA MWINGINE UJUMBE HUU ILI AJIHADHARI YASIJE KUMKUTA AKAJA KULIA NA KUSAGA MENO. WAKORA WAITU!
HABARI HII NI KWA HISANI YA MDAU BENJAMIN NKILA
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
on Thursday, September 6, 2012
Post a Comment