Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali leo July 19, 2012.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Bi Salome Abeli, mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission jijini Arusha, aliyekuwa njiani kuelekea Pemba kikazi kabla ya kupatwa na ajali hiyo ya meli. Amesema hali yake inaendelea vyema hapo katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Post a Comment