Mara nyingi katika maisha yetu ya
kila siku tumesikia sana maneno kama “nipe tano” “chukua tano” maneno haya
yamekuwa maarufu sana na katika mazingira tofauti maneno haya yamekuwa yakiashiria
ushindi, au hali ya mafanikio au furaha baada ya hali fulani. Vivyo hivyo
katika maisha yetu ya kutafuta kufanikiwa katika yaleyote tunayoyafanya
kilasiku viko vitu au ziko hatua ambazo huwa zinatulazimu kuzijua au kuzipitia
kama kweli tunamaanisha na tunayadhamiria hayo mafanikio tunayoyatafuta. Ni
ukweli kwamba watu wengi hutamani sana mafanikio na kuyazungumzia sana katika
maneno yao ya kilasiku lakini kwa bahati mbaya hawajawahi kuyaishi mafanikio
hayo kwasababu ya kutokuwa na dhamira madhubuti katika kuyaelekea mafanikio
hayo. Kama ambavyo tunaposema “high five” tunagonga mikono yetu na vidole vyetu
vitano vikiwa vimefunguka kuashiria ushindi basi vivyohivyo nitajaribu kugusia
hatua tano au vitu vitano vitakavyokusaidia kugonga mkono wa “ high five” baada
ya kuyafikia mafanikio yako. Kwakifupi vitu hivyo ni,
Uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyo navyo
ndani yako.
Uwezo wa kusimama au kuwa na msimamo.
Uwezo wakujitengenezea sura ya maisha yako.
Na uwezo wa kuyaongoza maisha yako.
Fuatana na mimi katika kuzichambua hatua hizi
hapa chini.
1. Kuwa na uwezo binafsi wa kuvikagua
vile ulivyonavyo ndani yako (Take a stock)
Katika maisha yetu ya kilasiku
hatunabudi kujifunza namna ya kujikagua sisi wenyewe, kuvikagua vile
tulivyonavyo ndani yetu kwasababu ni ukweli kwamba pasipo kujikagua sisi
wenyewe basi hatutaweza kuyatambua mapungufu tuliyonayo na kama hatutoyatambua
mapungufu tuliyonayo basi mapungufu hayo hayatoweza kushuhulikiwa na kuondolewa,
maana yake ni kwamba tutazidi kuishi na mapungufu yetu na hivyo kuathiri
ufanisi wetu na mwisho wake mafanikio yetu kwa ujumla yataathirika. Labda
nikupe mfano wa mtu mwenye duka, mara kwa mara mmiliki wa duka huwa na muda wa
kuvikagua vitu au mali aliyonayo dukani (stock taking) na hapa huwezakutambua
nini kimepungua, nini hakipo kabisa na nini kipo kwa wingi. Katika kujikagua
sisi wenyewe sio tu tunapata uhakika wa vile tusivyonavyo (weaknesses) bali pia
tunapata kufahamu vile tulivyonavyo kwa wingi (strengths). Jifunze kufanya
tathmini ya maisha yako binafsi kila wakati, tathmini matendo yako ya kilasiku,
maneno yako ya kilasiku, mitazamo yako (perceptions and attitudes) halafu
angalia wapi kuna mapungufu na wapi kuna fursa zaidi). Baadhi ya mapungufu
ambayo twaweza kuwa nayo katika maisha ni kama vile mapungufu ya kihisia
(emotional gaps), mapungufu ya kiroho (spiritual gaps), mapungufu ya kiujuzi
(skills gaps), mapungufu ya kifedha (financial gaps) na mengineyo mengi.
Kumbuka, uzuri ni kwamba kila tunapoweza kuyatambua mapungufu haya tunaziona
fursa za kuweza kuyashuhulikia.
2. Uwezo wa
kuwa na msimamo (Take a stand)
Wengi wetu tumeshindwa kuyafikia
malengo tuliyowahi kujiwekea kwasababu tu hatuna misimamo katika vile
tunavyoviamini kwahiyo inakuwa rahisi kuyumbishwa na kupeperushwa na kila upepo unaokuja upande wetu. Ili kufikia
mafanikio tunayoyatamani hatunabudi kuwa na misimamo fulani katika maisha.
Naupenda msemo unaosema kama huwezi kuwa na msimamo katika chochote basi
utachukuliwa na chochote “He who stands for nothing will fall for anything”.
Kama wewe ni kijana na huna msimamo katika chochote basi ni rahisi kujikuta
unachukuliwa na vingine ikiwemo madawa ya kulevya, umalaya n.k. Kama wewe ni
mfanyakazi na hauna msimamo katika baadhi ya mambo basi ni rahisi kujikuta
unabebwa na mengi kama vile rushwa na ubadhilifu. Ni vema kufahamu kila wakati
maishani kuwa kama hauna msimamo katika ufanisi basi utaangukia katika uzembe
na kutowajibika, na kama hautakuwa na msimamo katika kuhakikisha unafanikiwa
basi utaangukia katika umaskini.
Kusimamia kitu fulani
maanayake ni kuwa na nidhamu, kujua kanuni, na kukiheshimu kitu kile
unachokisimamia. Kanuni na nidhamu hizi ndizo zinazotuongoza katika maisha yetu
ya kilasiku katika kufikia kile tunachotamani. Amua mwenyewe ninini unasimamia
na ni wapi unaiweka misimamo yako kwasababu vile tunavyoamua kuwa na misimamo
navyo ndivyo vinavyosimama kama misingi katika maisha yetu.
3. Uwezo wakupiga hatua
(Take a step)
Yamkini unatamani sana kufanikiwa na
kilasiku unaongelea sana mafanikio, ni vema kujua kwamba mafanikio yetu hayaji
kwa kuyatamani sana au kuyaongelea sana bali katika uwezo binafsi wa kuamua
kupiga hatua. Yawezekana uko katika chombo kizuri tu cha usafiri lakini
utajikuta unapitwa na kila mtu, hata wale wenye vyombo vibovu vya usafiri nao
watakupita kama utakuwa umekaa tu kwenye chombo chako pasipo kuruhusu mwendo.
Chukua hatua kuelekea mustakabali wako, angalia mbele yako unaona nini? nini
ambacho unakiona kwenye mustakabali wako? Nini ungetamani ukipate kwenye
mustakabali wako? Anza kufanya kila kinachohusika ili kuiona hiyo ndoto yako
ikiwa dhahiri. Anza kupiga hatua ya kwanza na hatua nyingine zitakuwa rahisi
kufuatia. Kamwe usitishike na umbali unaouona kuelekea mustakabali wako, jinsi
unavyopiga hatua ujasiri wako unafunguka na kukua, kumbuka kuwa kila hatua
unayoipiga hatakama nindogo kiasi gani inakusogeza karibu na mustakabali wako.
Usisahau tu kuwa ziko mbio unatakiwa kuzikimbia na uko ushindi unatakiwa
kuushinda ilikufikia hapo unapotamani, kwahiyo piga hatua.
4. Uwezo wa kujitengenezea
sura ya maisha yako (Take a shape)
Katika maisha yetu ya kilasiku ni
ama uamue kuitengeneza sura ya maisha yako au kuibomoa sura hiyo, wengine wetu
maisha yetu hayajawahi kuwa na sura nzuri ya kuvutia, sisi wenyewe ndiyo wenye uwezo
wakuamua kuitengeneza sura hiyo kuwa vile tunataka iwe, ukiamua kukaa tu pasipo
kufanya chochote basi umekusudia kwa dhamira halisi kuiharibu sura ya maisha
yako mwenyewe. Ulimwengu waleo unabadilika kwa kasi sana, ili kuweza kubakia
wenye maana na wenye umuhimu basi hatuna budi kuwezana na mabadiliko hayo. Kama
hatutoweza kuyaweza mabadiliko ya karne hii basi mabadiliko hayo yatatuweza
sisi (If you don’t manage change change will mismanage you). Fahamu dhahiri
kwamba karne ya 21 haijaleta tu fursa bali na changamoto tele.
Lazima tuweze na tuwe na ujuzi wa
kufanya tabia zetu za kilasiku kuendana na mabadiliko haya, lazima kuwa kasi
kama vile kasi ya mabadiliko ilivyo, lazima kuwa wenye uwezo wa kuendana na
mazingira kwasababu ukijaribu kukakamaa na kutokubali mabadiliko (being rigid)
katika enzi hizi basi lazima utavunjika. Chamsingi wote tujitahidi kufanya hata
yale ambayo maranyingine hayaturidhishi sana, yale ambayo tunaona yanatugarimu
zaidi na kutuminya zaidi, kumbuka mafanikio sio wakati wote yanakuja tukiwa
tunayasubiria kwa kicheko bali maranyingine kwa kuumia (we must be willing to
step out of our comfort zones)
5. Uwezo wa kukikalia kiti
na kuyaongoza maisha yako mwenyewe (Take a seat)
Ziko nyakati ambazo wengi wetu hatuwezi
kufika tunapotamani kufika kwasababu dereva anayeendesha chombo chako sio wewe,
wakati huohuo unafikiria kuelekea pale unapotamani wewe. Ningumu sana. Katika
maisha kama kweli unaifahamu ndoto yako na unaiona kesho yako na unaitamani
sana kuifikia basi amua kukaa kwenye kiti cha dereva wewe mwenyewe na kuendesha
chombo kuelekea huko. Wengi wetu sio kwamba tumewakabidhi wengine udereva wa
safari yetu kwa kujua bali kwa kutokujua, mara unaona muelekeo wa safari sio
ule ulioutarajia, yamkini sasa dereva uliyemkabidhi kiti anakupeleka kwenye
ndoto yake siyo yakwako tena. Sasa amuakuingia kwenye kiti cha dereva wewe
mwenyewe, hayo ni maisha yako na siyo ya mwingine. Kamwe usiache furaha na
mafanikio yako katika mikono ya wengine. Kubali na kuwa tayari kubeba
majukumu. Kama inatokea unafanya makosa basi usijitetee na kukwepa, kwasababu
kujitetea na kukwepa yawezakuwa njia tu ya kuchomoka na siyo njia ya kuendelea
mbele. Usiwalaumu wengine kwa madhaifu na kushindwa kwako, kwasababu kwa
kufanya hivyo unaipoteza nguvu ya kukua. Chukua tano!!!!
Acknowledgement: Dr John Tibane’s
teachings.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
on Sunday, July 8, 2012
Post a Comment