Social Icons

Loading...

CHEZEA MNYAMA WEWEEE; ATAFUNA AZAM BAO 4 - 3.

SIMBA AKITAFUNA KONI ZA AZAM


"Mnyama" Simba SC leo imesasambua vilivyo timu ya Azam FC katika fainali ya kombe la Urafiki. Mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam na kwa mara ya kwanza ukichezeshwa na marefa wote toka Zanzibar kwa kushinda kwa penati 4 -3. Simba iliyotawala sana kipindi cha kwanza na kufanikiwa kutupia kambani bao la kuongoza kupitia kwa Mzambia Felix Sunzu ktk dakika za mwanzoni; lakini katika dakika ya 43 kipindi hicho Azam Fc walirudisha bao hilo kwa kichwa kupitia kwa Hamis Mcha "Vialli" na hivyo kipindi cha kwanza kuisha kwa timu hizo kuwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilianza kwa Azam Fc kulishambulia lango la Simba kama nyuki na kufanikiwa kutupia kambani bao la pili kwa kichwa kupitia kwa John Bocco Adebayor.

Simba ambayo ilionekana imekata tamaa na kuishiwa pumzi ilifufuka ghafla baada ya kufanya mabadiliko ambapo kocha Prof. Milovan Curcovic aliwaingiza  Danny Mrwanda, Haruna Moshi "Boban" na Uhuru Suleiman. Mabadiliko haya yaliisaidia Simba kwani walifanikiwa kurudisha bao hilo kupitia kwa Mwinyi Kazimoto baada ya kupiga penati iliyotolewa baada ya Danny Mrwanda ambaye alikuwa ameichomoka beki ya Azam Fc na hivyo Ibrahim Shikanda akamkwatua ndani ya eneo la penati. Bao hili lilifanya dakika 90 kuisha kwa sare ya 2-2.

Manahodha na marefa walikubaliana mapigo ya penati "Matuta" yapigwe ili kumpata mshindi. Simba ilianza kupata penati ya kwanza kupitia kwa Mwinyi Kazimoto huku penati iliyofuata ikipigwa na Haruna Moshi ambaye alikosa penati wakati Azam Fc wao walipata penati 3 na kukosa 2 ambapo Juma Kaseja aliendelea kuonyesha umwamba wake kwa kunyaka kistadi mkwaju wa mwisho wa Azam Fc.  Hivyo kuipa nafasi Simba kutupia kabatini kombe la pili kwa mwaka huu wa 2012. Huu ni mwanzo mzuri na ishara nzuri kocha Milovan Circovic na kikosi chake hasa wakati huu inapojiandaa na kombe la Kagame (Kombe la Africa Mashariki na Kati). Kombe hili litatia hamasa na hali mpya ya ushindi.

Simba na Azam Fc zitapambana tena katika ngao ya hisani kufungua pazia la ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mwaka wa 2012/2013. HONGERA SIMBA...WEMBE NI HUO HUO CHARAZA TIMU ZOTE NA LETA HESHIMA YA TANZANIA KWENYE KOMBE LA KAGAME.  

BAADA YA KUMTAFUNA  "KWA MBINDE" AZAM FC "MNYAMA" ANAWAFUKUZIA MAADUI ZAKE KWENYE KOMBE LA KAGAME...YANGA MUPOOOOOOO?

Waziri asiye na Wizara maalum wa Zanzibar, Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma

 

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top