Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya
Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Dr.
Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika
klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka
aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na
kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu
wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi
aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi
Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio
hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba
wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za
kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.
chanzo: http://www.fullshangweblog.com/
Post a Comment