Vifo, uharibifu wa mali, miundombinu na mafuriko, msongamano wa
magari, baadhi ya wakazi wa jiji hilo kukimbia makazi yao, wengine
kulala kwenye magari na nyumba za wageni vimewakumba wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam na vitongoji vyake, kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha kwa siku ya nne mfululizo.
Uukoaji ukiendelea .
Sehemu ya barabara iliyoharibika katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo
Timu ya waandishi wa gazeti hili walifanya
uchunguzi maeneo mbalimbali na kushuhudia hali halisi ilivyo, huku
wanawake na watoto wakionekana kupata shida zaidi kwa kukaa nje ya
nyumba zao, wengine kuhamia kwenye majengo ya shule.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
alisema jana kuwa walikuwa wakiendelea kukusanya taarifa za maafa
ikiwamo vifo alivyosema ni vingi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik alisema kuwa yupo kwenye kikao na watatoa taarifa zaidi za maafa baadaye.
Kijana ambaye akufahamika jina lake akijaribu kuokoa maisha ya akina mama waliotaka kusombwa na mafuriko jijini Dar es salaam
Kijana ambaye akufahamika jina lake akijaribu kuokoa maisha ya akina mama waliotaka kusombwa na mafuriko jijini Dar es salaam
Tegeta, Boko na Bunju
Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne,
amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kujaa maji na
kushindwa kujiokoa kutokana na ulemavu, wakati mama yake akiwa kwenye
shughuli za biashara.
Majirani wa mtoto huyo walisema tofauti na kawaida
yao kumtoa mtoto huyo mvua inaponyesha, jana walimsahau na mama yake
aliporejea alikuta maiti ya mtoto wake ikielea chumbani.
Katika mvua hizo takribani kaya 180 zimekumbwa na mafuriko huku wakazi wake wakijikuta hawana pa kwenda.
“Mimi nimekuwa hapa tangu Tanu imezaliwa, nyumba
yangu imejaa maji nimeshazeeka sina mtu wa kunisaidia, wala sijui wapi
nitakwenda. Nomba Serikali inisaidie,”alisema Hussein Ngaoma ambaye ni
mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo.
Naye Husna Ally ambaye pia nyumba yake imekumbwa
na mafuriko alisema: “Nasikitika, maana nimepata hasara kubwa. Mimi ni
mfanyabiashara katika eneo hili la Boko, nina duka la kuuzia samani
limejaa maji na sijaweza kuokoa chochote. Mzigo wa Sh30 milioni
umeharibika wote.”
Jeti Lumo
Katika eneo hilo licha ya kujaa maji, mfanyabiashara ndogondogo amefariki dunia kwa kusombwa na maji Uukoaji ukiendelea .
Post a Comment