TAFITI za kisayansi zimebaini kuwa nguo za ndani hasa zinazobana
kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa
mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi za
Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la
Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na
zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume
(manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.
Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya
kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti
nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za
kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke.
Akizungumzia utafiti huo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, alisema una ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.

“Kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” alisema Dk Massawe.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1639126/-/11pbn3f/-/index.html
Post a Comment