TANGU Serikali ya Tanzania iridhie pikipiki maarufu kama bodaboda kubeba
abiria, tumeshuhudia ndugu na marafiki zetu wakipoteza maisha na hakuna
ubishi sasa ni janga la kitaifa.Inavyoonekana, wakati Serikali
ikiruhusu pikipiki kubeba abiria ilikuwa haijajiandaa kikamilifu na
badala yake ilijikita kuangalia mapato ya kodi yatakayotokana na
biashara ya kubeba abiria na kikubwa zaidi kutengeneza ajira kwa vijana.Naamini
Serikali haikujiandaa kwa sababu leo hii si ajabu kijana kujifunza
pikipiki kwa dakika 30 na kuingia barabarani kubeba abiria. Serikali iko
kimya!.
Takwimu zinatuonyesha tangu 2009 serikali ilipokubali pikipiki kubeba abiria mpaka mwaka jana, pikipiki 330,882 zimesajiliwa nchini sawa na asilimia 60 ya usafiri huo.
Ongezeko hilo la pikipiki limekuja na janga lingine kwa Watanzania. Vifo na majeruhi wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na kuwasababishia baadhi ya vijana na abiria ulemavu wa kudumu. Sababu kubwa ya vijana na abiria wa pikipiki kupata ulemavu wa kudumu ni uzembe wa madereva uchwara kufanya kazi hiyo.Tunaambiwa mwaka 2011 pekee, kulikuwapo ajali 5,384 za pikipiki zilizosababisha vifo vya watu 945 na majeruhi 5,506, wakati mwaka 2010 kuliwapo ajali 4,463 zilizosababisha vifo vya watu 683 na majeruhi 4,471.Takwimu za hivi karibuni kabisa–Januari mpaka Septemba 2012 kulikuwapo ajali za pikipiki 4,142 zilizosababisha vifo 720 na kuwaacha Watanzania wenzetu 4,057 wakiwa walemavu.
Kwa habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/uchambuzi/-/1597604/1636696/-/mm5rjvz/-/index.html

Post a Comment