Kikosi cha Yanga kilichoifunga Azam 2 -0, magoli yaliyofungwa na Didier Kavumbangu na Hamis Kiiza. |
Yanga ilmewakilishwa
Ally Mustafa Barthez, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Naroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.
Kikosi cha Azam FC. |
Nako huko Morogoro.
Kutoka mjini
Morogoro Simba ya jijini Dar es Salaam leo imejikuta ikiangukia pua
baada ya kuchapwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, mchezo litawaliwa na rabsha
za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa
Simba waliokuwa na hasira wakidai mwamuzi Judith Gamba, alikuwa
hawatendei
haki.
Mtibwa
ilijipatia bao dakika ya 34, kwa bao lililofungwa na Mohamed Mkopi baada ya
Kipa Juma Kaseja kutema shuti kali la Vicent Barnabas.
Dakika
ya 87, mshambuliaji mahiri Hussein Javu, aliipatia Mtibwa bao la pili, baada ya
Kaseja kufanya mbwembwe langoni mwake.
Baada
ya mchezo kumalizika, Kaseja aliangua kilio uwanjani huku mashabiki wakimzonga.
Wachezaji wa Simba waligoma kupanda basi lao, ambako baadhi
ya viongozi wao walifanya kazi ya ziada kuwabembeleza, ambako walikubali kwa
shingo upande, lakini baada ya muda Mrisho Ngasa alishuka akiwa kabadilisha
nguo kuondoka kivyake huku akisindikizwa na mashabiki lukuki.
Kwa
matokeo ya mechii za leo, Yanga imekamata usukani rasmi ikiwa na pointi 26 huku Simba
ikibaki na pointi zake 23 wote wakiwa na michezo 12 huku Azam ikiwa nafasi ya
tatu kwa pointi 21 huku Mtibwa ikifikisha pointi 13.
Post a Comment