TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amemteua Vuai Mwinyi
Mohammed kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar
Dkt. Abdul hamid Yahya Mzee imesema kuwa Rais Shein amefanya uteuzi huo kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya
Mwaka 1984
Aidha Dkt. Shein amewateua
Ameir Ali Khatib kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Rais(Mnukulu) Ikulu katika Ofisi
ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.Pia Rais amemteua Makame
Ali Makame kuwa Mkurugenzi wa Mipango,Sera na Utafiti katika Wizara ya Miundo
mbinu na Mawasiliano, Zanzibar.
Halikadhalika Dkt Shein
amemteua Mariyam Juma Abdalla Saadalla kuwa Mkurugenzi wa Mipango,Sera na
Utafiti katika Wizara ya Kilimo na Maliasili,Zanzibar .
Vile vile Dkt Shein
amemteua Mwalim Hamad Mbarouk kuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani katika Wizara
ya Ardhi,Makaazi, Maji na Nishati,Zanzibar.
Rais amefanya uteuzi huo
kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984Uteuzi huo wote
unaanza leo.
Pia
Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzíbar amemteua Sebtuu
Mohammed Nassor kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani ya
Zanzíbar.
Rais maefanya
uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha Sheria ya Baraza la
Mitihani la Zanzíbar namba 6 ya 2012
Uteuzi huo
umeanza tarehe 31 Oktoba 2012
Wakati huo huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir
amewateua Wajumbe wa Bodi ya Utumishi ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Uteuzi huo
umefanywa kwa mujibu wa Sheria namba 11 ya Mwaka 2003 iliyoanzishwa Ofisi ya
mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kifungu cha 8(1)
kinachoanzisha Bodi ya Utumishi ya Ukaguzi.
Walioteuliwa ni
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini Othman Bakar Othman ambaye atakuwa
Makamo Mweneykiti wa Bodi hiyo.
Fatma Mohammed
Said ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameteuliwa kuwa
Mjumbe wa Bodi.
Wajumbe wengine
wa Bodi hiyo ni Fatma Saleh Amour kutoka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu,
Abdalla Mohamed
Mbwana na Tafana Kassim Mzee.
Uteuzi wa
Wajumbe hao umekuja baada ya Rais wa Zanzibar kumteua Amina Juma Zidikheri kuwa
Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Uteuzi huo
umeanza Oktoba 27,2012
IMETOLEWA NA IDARA
YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 02/11/2012
Post a Comment