UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewateuwa
Davis Mosha, Muzamili Katunzi na Beda Tindwa katika kamati ya Mashindano
huku Baraka Kizunguti akiwa Ofisa Habari na Shaban Katwila akiwa Meneja
wa timu hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kuwa maamuzi hayo yametolewa katika kikao cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo.Alisema waliouteliwa wataanza kazi zao mara moja katika klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na kujulishwa uteuzi huo.Mwalusako alisema licha ya kuwepo kwa maamuzi hayo Kamati hiyo imepanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama ambao utafanyika Desemba 16 mwaka huu.Alisema Mkutano huo utafanyika kama kanuni za klabu hiyo zinavyosema ambapo kila mwaka ni lazima ufanyike mkutano wa wanachama kujua maendelea na klabu yao.
"Hayo ndiyo maamuzi ya Kikao cha
Kamati ya Utendaji....ambapo kina Mosha watakuwa chini ya Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Abdallah Bin Kleb na Mkutano Mkuu utafanyika Disemba
16"alisema Mwalusako.Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa klabu hiyo
Ernie Brandts, ameipongeza timu yake kwa kuweza kupata ushindi katika
mchezo wao wa juzi ikiwa ni pamoja na kufikia malengo yake.Akizungumza Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kuwa maamuzi hayo yametolewa katika kikao cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo.Alisema waliouteliwa wataanza kazi zao mara moja katika klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na kujulishwa uteuzi huo.Mwalusako alisema licha ya kuwepo kwa maamuzi hayo Kamati hiyo imepanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama ambao utafanyika Desemba 16 mwaka huu.Alisema Mkutano huo utafanyika kama kanuni za klabu hiyo zinavyosema ambapo kila mwaka ni lazima ufanyike mkutano wa wanachama kujua maendelea na klabu yao.
Akizungumza mara baada ya mchezo wao dhidi ya Azam, kocha huyo alisema amefurahishwa na uwezo wakliionesha wachezaji wake katika mchezo huo ikiwa ni pamoja na kupata mabao 2-0.Brandts alisema kwa kiwango alichokiona jana ni wazi wachezaji wake wamejipanga kuifikisha mbali timu yake ikiwa ni pamoja na kufikia malengo alijiwekea.
"Nimefurahishwa sana na uwezo wa leo ikiwa ni pamoja na kupata ushindi mnono kwa timu ngumu kama Azam ambayo hucheza mchezo mzuri kila mara"alisema Brandts.
Post a Comment