Social Icons

Loading...

Muhongo,Sitaomba radhi kwa wezi.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameapa kuwa kamwe hataomba radhi bunge kwa madai aliyotoa dhidi ya watu aliowatuhumu kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao amewafananisha na wezi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi juzi, Profesa Muhongo alisema yote aliyoyasema kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kilichopita ni sahihi na ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.
“Kamwe sitaomba radhi kwa wezi. Subirini muone na kusikiliza kwenye kikao kijacho cha Bunge nitakachoongea kwa muda wa hizo dakika tano wanazotaka kunipa niombe radhi,” alisema Profesa Muhongo.
Alitoa kauli hiyo alipotakiwa kuzungumzia kuvuja kwa ripoti ya Kamati ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuchunguza tuhuma za rushwa kwa wabunge zilizosababisha Kamati ya Nishati na Madini kuvunjwa.
Taarifa hizo za kuvuja kwa ripoti hiyo zinaeleza kuwa, Kamati ya Ngwilizi imependekeza Waziri aombe radhi na Katibu Mkuu wa wizara yake, Eliakim Maswi achukuliwe hatua za nidhami na mamlaka zilizo juu yake.
“Yaani watu waibie taifa, tuwagundue na kuwasema, halafu nisimame kuowaomba radhi? Sitafanya hivyo. Sitaki kuzungumza mengi, lakini Watanzania wasubiri kauli yangu siku jambo hilo litakapowekwa hadharani,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Soma  Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/biashara/13-biashara-za-kitaifa/26765-muhongo-sitaomba-radhi-kwa-wezi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top