TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE
TANZANIA (PCT)
Tarehe 25/10/2012
Ndugu wapendwa Wakristona Watanzania wenzetu kwa ujumla,tunawasalimu katika Jina la Bwana WetuYesu Kristo.Itakumbukwa kuwasikuyaterehe 12/10/2012 sote tulishitushwa na ghasia za kuchomwa kwa makanisa,
Biblia Kuchanwa, kupigwa watumishi wa Mungu, kubomolewa kwa makanisa na
sehemu takatifu za ibada yaani madhabahu kukojolewa;uhalifua mbao
ulifanyika huko Mbagala jijini Dar es Salaam.
Pamoja na juhudi za Serikali yetu
kupitia Jeshi la Polisi kufanya kazi ya kurejesha amani na utulivu
Nchini, sisi .Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste
tumesikitishwa na kitendo cha watoto waliohusika na kitendo cha
kukojolea Quran (mtotowa Kikristo aliyekojolea Juzuu pamoja na mwenzake wakiislamu aliyemchochea kufanya kitendo hicho);pia
tumehuzunishwa na kufadhaishwa zaidi baada ya kusikia tamko la serikali
kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani kuwa waliohusika na uvunjaji wa
makanisa ni wahuni.
Kwa mtazamo wetu kama viongozi wa dini tunaona kauli ya serikali inamaanisha kuwa, SerikaliHaiamini kwamba waliohusika na
uvunjaji wa makanisa,kuchoma Biblia,kubomoa na kukojolea
madhabahu,kunywa na kula mikate ya meza ya BWANA pamoja na kuwapiga
watumishi wa Mungu ni wanaosadikiwa kuwa ni wanaharakati wa kidini;bali
ni
Wahuni
tu.Kimsingi, utafiti uliofanywa na baraza letu unaonyesha kuwa vitendo
hivi havikufanywa na wahuni bali wanaharakati wakidini
Kwa sababu zifuatazo:-
1. Mkusanyiko
wa watu waliofanya uhalifu katika makanisa ulianzia msikitini baada ya
sala ya adhuhuri, ukaelekea katika kituo cha Polisi ambapo mtuhumiwa wa
kukojolea Juzuu alikuwa amehifadhiwa, na wakataka wapatiwe(kijana huyo anayetuhumiwa) ili wamwadhibu kwa mujibu wa sharia’h za kiislamu kwani walidai ameidhalilisha Qurani Tukufu.
2. Uhalifu wa Kuchomwa kwa makanisa ni moja ya utekelezwaji wa hotuba na maandishi ya wanaharakati (Fisabih Lilah) yanayowahimiza
baadhi ya waislamu kudai haki zao za kutaka kujikomboa na Kanisa na
Ukristo ambao wanadai ni matokeo ya ukoloni, na kwamba Tanzania
inatawaliwa na mfumo wa Kikristo ambao umetapakaa kama damu mwilini
kuanzia ngazi ya juu ya utawala wa nchi hadi chini kwa jina maarufu
“MfumoKristo”(Tunao ushahidi wa hotuba na mafundisho ya wanaharakati katika CD, DVD na magazeti).
Inashangaza
kuona serikali ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia ulinzi na usalama
wa raia na mali zao; kupuuza madai haya na kushindwa kabisa kuzuia
uhalifu wa matukio ya kuchomwa makanisa ambayo kimsingi ya nafanana
kwani yalishatokea huko Zanzibar, Bagamoyo, Tunduru, Mwanza, Ndanda,
Rufiji, Kigoma, Mto wa Mbu na sasa Mbagala;kwa kisingizio cha kuwaita
wanaofanya matukio hayo kuwa ni wahuni.
Kwa kuwa ni wajibu wa serikali
kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba
utu na haki nyinginezo zote za binadamu zina heshimiwa na kuthaminiwa,
Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania tungependa
kuishauri Serikali yetu mambo yafuatayo:-
1. Irejee misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri Ya Mungano waTanzania ambayo inatamka wazi kuwa; “Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia isiyokuwa na Dini”[KatibaYa 1977, Ibara ya 3 (1)].Hii
itasaidia kuondoa hisia za kundi moja la Dini kuona idadi kubwa ya
Viongozi na watawala waliopo madarakani pamoja na wakuu wa Vyombo vya
ulinzi na usalama wako upande wadini Fulani.
2. Serikali
kwa kushirikisha mabaraza yote ya kidini Nchini iundeTume huru itakayo
kuwa najukumu la kusimamia na kuishauri serikali juu ya uendeshwaji wa
shughuli za taasisi na jumuiya za kidini nchini. Jambo hili litasadia
kubainisha mipaka ya kiutendaji kati ya uendeshwaji wa shughuli za
kidini na mamlaka ya Nchi ambao umetajwa kwa wazi katika Katiba Ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ya 1977, ibara 19 (2);na hivyo kuondoa
dhana ya kutaka kuingiza “udini” kwenye siasa ambayo inaelekea kuota
mizizi Nchini.
3. Hata
hivyo,baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania tunatoa tamko kulaani
uvunjifu waamani ambao umejitokeza kupitia vurugu zilizojitokeza hivi
karibuni Nchini, na tuna waomba waumini wetu waendelee kudumisha hali
ya utulivu na amani ambao umejengwa na waasisi wetu tangu Uhuru wa Nchi
yetu; japo sote tunajua kuwa haki yetu ya kufanya ibada tuliyopewa na
Mungu inaelekea kuvunjwa na watu wengine wasioheshimu uhuru wa ma wazo
na imani katika dini. Nawafahamu kuwa yuko aliye juu kupita walio juu
ambaye anayaona haya yote yanayotendeka.
Kwa ndugu zetu wanaoitwa
Wanaharakati wa Kiisalamu, sisi tunajua imani yenu na mtazamo wenu
kuhusu Wakristo; pamoja na msimamo mlionao juu ya kitabu cha Quran na
juu ya kupigania Dini ya allah (subhahanahu wataa’alah); lakini
kwa kuwa sote ni Watanzania tunawakumbusha kuwa jukumu la kudumisha
amani ya Nchi yetu ni letu wote; hivyo, tutumie busara zetu katika
kudumisha stahmala inayokazia kuheshimu hisia za watu wengine
katika masuala ya kiimani kwani kutokufanya hivyo ni kuhalifu sheria
tuliyojiwekea sisi wenyewe.
Aidha, Baraza la Makanisa ya
Kipentekoste linaitaka serikali isisite kutoa tamko kali pindi vurugu za
kidini zinapojitokeza bali iendelee kushughulikia migogoro ambayo
inaweza kusababisha tena vurugu za kidini kwa nguvu zake zote, na
iwabane waliohusika na uvunjajiwa makanisa warejeshe mali wakizochukua
na kulipafidia za uharibifu wa kuchoma makanisa 10 Tanzania bara na
jukwaa moja kwani kwa kufanya hivi itawahakikishia Watanzania kuwa hali
hii haijitokez atena.Kwa matukio haya ya kuchomwa makanisa Nchini,
Serikali yetu itambue kuwamacho na masikio ya wapenda amani Nchini na
Ulimwenguni pote wanasubiri kwa hamu kuona ni hatua gani madhubuti
serikali itachukua kwa watuhumiwa wa matukio ya uvunjwaji wa makanisa
yaliyofanyika huko Zanzibar na Tanzania bara............................... .............................. .......
Askofu Davidi Andulile Mwasota
Katibu Mkuu PCT Taifa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA ILI IZIDI KUWA KISIWA CHA USALAMA NA AMANI.
Post a Comment