Social Icons

Loading...

DAR KWAZIZIMA, ZANZIBAR KWALIPUKA .

Baadhi ya maeneo ya mjini Zanzibar na waandamanaji wa "UAMSHO"
Wakati vurugu za kidini zikianza kushika kasi katika nchi inayoaminika kuwa ni kisiwa cha amani Dunia Tanzania, hali ya kizungumkuti na sintofahamu ya utulivu na amani iliyodumu kwa zaidi ya miaka hamsini yaelekea halijojo kwani hamkani si shwari sasa nchini kutokana na mivurugano ya kidini iliyoanza kudhihirika waziwazi hivi karibuni baada ya mtoto mmoja huko Mbagala kusemekana amekojolea quran.
Chokochoko hizi za kidini zilizonakshiwa na siasa za "majitaka" zimeanza siku nyingi na sasa zimepata mashiko haswaa kila kona ya nchi hasa tukikumbuka kwamba ni wiki chache zilizopita huko Tunduru kanisa moja lilichomwa moto na gari la mchungaji kuunguzwa kama hiyo haitoshi baadhi ya makanisa yalitiwa kiberiti mchana kweupe huko Zanzibar huku wenye dhamana ya ulinzi na usalama kutochukua hatua za kuzima mashambulizi hayo. Ndani ya wiki hii vurugu hizo zimeendelea ambapo tumeshuhudia huko Kigoma kanisa lingine likichomwa moto jumapili hii;  wakati huko Mbagala makanisa mbalimbali yakichomwa, magari vitu na samani nyinginezo vikichiomwa na vingine kuibiwa. Yakadiriwa zaidi ya shilingi Bilioni 1 zimeteketea kutokana na machafuko hayo.
 Jana takribani watu 36 walitiwa korokoloni na kufunguliwa mashtaka kwa kuwa chanzo cha vurugu na uharibifu wa mali za watu.

Mmoja wa wafuasi wa dini ya kiislamu akipelekwa kituo cha kati cha polisi DAR


Vurugu hizo zimezidi zaidi baada ya polisi kumtia mbaroni Katibu wa Jumuiya na taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda. Wafuasi wa Sheikh Ponda mchan wa leo Jumatano wameandamana katika mitaa ya Kariakoo na Posta mjini Dar Es Salaam wakishinikiza kiongozi wao huyo na wafuasi wengine wanaotuhumiwa kuchoma makanisa waachiwe huru.  

Habari zilizovuja ziansema kwamba Sheikh Ponda ametiwa mbaroni kwa kuonekana kama ndiye kiongozi na mshawishi mkubwa wa maandamano na uchomaji wa makanisa hapa nchini.
Yasemekana kwamba Sheikh Ponda amesambaza waraka wa kichochezi wa kidini ambao unahamasisha chuki baina ya wakristo na waislamu na pia serikali na wakristo na hata taasisi zingine za kiraia za kutetea haki za binadamu. Waraka huo ambao blog yetu pia imeupata unaelezea kwa kina michakato mbalimbali na shutuma ambazo waandishi wanadai na kuhamasisha waislamu waamke sasa.


ZANZIBAR NAKO KWAWAKA MOTO
 Wakati katika Jiji la Dar Es Salaam hali si shwari huko Zanzibar eneo la Darajani leo lilifungwa kwa muda baada ya kuzuka tafrani na uchomaji wa moto kwa kile kilichodaiwa kuwa kundi la waislamu la "UAMSHO" liliingia mtaani na ghasia kubwa kuzuka na polisi kuingilia kati.

Moto mkubwa uliwashwa na waandamaji na hivyo kufunga barabara yote katika eneo la Darajani, Zanzibar.



Kikosi cha kuzuia ghasia ilibidi kiingilie kati kuzuia uharibufu wa mali na vitu na uvunjifu wa amani kisiwani humo hii leo jumatano.

 Vikosi  vya  usalama   wakiwa katika  Doria  kutuliza  ghasia  .

Maskani ya   CCM      yachomwa  moto.


WAKATI HUO HUO...
Imesemekana kwamba kuna takribani vikosi vya wana UAMSHO katika meli mbili wako majini toka visiwani Zanzibar kwenda Dar Es Salaam mchana wa leo tayari kuungana na waandamanaji wengine ili kutetea wafuasi wao walitiwa korokoloni na jeshi la polisi lakini pia kuongeza nguvu kwa kile walichokiita "Mapambano ya kudai haki zao."

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

1 comments:

Waislamu hawana jipya! na kama hao ndo viongozi wanaowategemea kuwaonesha njia njema watapotea!
pigana vita ya kiroho sio ya damu na nyama!
wajiulize why hawajawahi sikia maandamano ya wakristo! kwani wao ndo wanajua Mungu!
Hata Biblia na Quran zinasema heshimuni mamlaka zilizowekwa!
wanatufanya wakristo tuamini uislamu sio dini ya kweli bali ni dini ya ushetani na fujo!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top