Social Icons

Loading...

Kimenuka ....Yanga wamtimua Kocha Mkuu.

Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga iliyoanza leo mchana baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika leo katika makao makuu ya klabu imeendelea imemkumbuka kocha mkuu wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet.

Taarifa za uhakika kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba  uongozi wa timu hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.

Mchana leo kamati ya utendaji ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari bila mpangilio wa klabu. Lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.

Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi hapo kesho.

Wakati huo huo aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda, wakati mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua amekabidhiwa majukumu ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye nae aliondolewa leo mchana.

Nafasi ya usemaji wa Yanga mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu
Taarifa  kwa  hisani  ya  Blog  ya  Shaffih 


 YANGA   YAICHEZESHA  KWATA  JKT  RUVU   4 -1  .......


Wachezaji Hamis Kiiza wa Yanga (kushoto), akiwania mpira na Ally Khan wa JKT Ruvu wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Yanga ikiwa na kocha wake msaidizi fred minziro imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Katika dakika kumi za mwisho wapenzi wa yanga walijikuta wakiomba mchezo umalizike baada ya jkt ruvu kucheza mchezo mkali. Wapenzi wa simba walionekana kushangilia hali hiyo ambayo hata hivyo matokeo yakawa 4-1.

Katika mchezo wa chamazi azam imeibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao la azam limepatikana dakika ya 26 ya mchezo kupitia kwa kipre tchetche.
Cledo mwaipopo ameipatia jkt ruvu bao moja baada ya kazi nzuri ya omar changa na sospeter manyasi.
  Yanga imepata bao la nne kupitia kwa didier kavumbangu baada ya kipa jkt ruvu kuutema mpira.
 dakika ya 52 simon msuva aliipatia yanga bao la tatu baada ya kuambaa ambaaa na mpira na kupachika wavuni. mapumziko yanga imetoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

 Bao la kwanza limepatikana dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa nadir haroub canavaro' baada ya kazi nzuri ya haruna niyonzima na athuman idd chuji
Dakika 31 yanga ilipata bao la pili kupitia kwa

didier kavumbagu akimalizia chuji. Katika kipindi cha kwanza yanga iliweza kutawala mchezo kwa kufanya mashambulizi mengi katika lango la jkt ruvu.

 Kwa upande wa jkt ikitumia wachezaji wake sospeter manyasi na omar changa walishindwa kufanya makeke makali hivyo mipira mingi kutoka nje.

  Kesho kuna mechi tatu ambapo mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita simba itavaana na Ruvu shootingStars mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa taifa dar es salaam. 
Mchezo mwingine utafanyika kwenye uwanja wa chamazi utazikutanisha african lyon dhidi ya tanzania prisons na mechi nyingine itakukuwa kwenye uwanja mkwakwani mkoani tanga mgambo jkt ikiwakaribisha. Kagera sugar. Kilatimu inahitaji pointi tatu ili iweze kukaa sawa katika msimamo wa ligi kuu.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top