KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia Kauli aliyoitoa mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza Silaha nchini.“Kauli hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya siasa inamshinda hivyo awaachie vijana” alisema Nape na kuongeza kwamba anatambua kuwa Uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza silaa kinyemela ni dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.
Chanzo: http://www.thehabari.com/habari-tanzania/ccm-dk-slaa-anazeeka-vibaya
Post a Comment