Social Icons

Loading...

Askofu Anapokuimbia “Nataka Nipate Lau Nafasï


 Ncheme  Nincheme  wa  Raia  Mwema
Haitarajiwi, katika hali ya kawaida, kwamba askofu wa kanisa anaweza kuwa anamwambia mke wa mtu’ “Napenda nipate lau nafasi/ Niweze kusema nawe kidogo, oh mama/ Rohoni naumia! Lakini hivyo ndivyo inavyokuwa mama wa watu akimpigia simu askofu akitaka kumuuliza jambo lo lote la kiimani, iwapo askofu anatumia simu yenye mwitikio wa wimbo huo wa Kilwa Jazz, ambao ni wimbo wa mapenzi.
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa kampuni za simu za mkononi kupandikiza sauti za miitikio wanayoiteua wao bila hata wateja wao kujua au kukubali. Kila aina ya miitikio imekuwa ikitumika, na ukimuuliza mwenye simu atakwambia hajui simu yake ina wimbo gani anapopokea simu.
Huu ni uvunjaji wa haki ya msingi kabisa ya mteja. Kama kuna wimbo au ujumbe wo wote ambao simu ya mteja inampa anayempigia simu mteja huyo, ni haki ya mteja siyo tu kujua huo ni wimbo au ujumbe gani, lakini pia akubali ujumbe huo au wimbo huo utumike kwa kutumia simu yake kama bango. Na pia, inatakiwa aseme kama angependa kulipwa kwa kutumika kama bango.
Tukiacha adha na mfadhaiko anaweza kupata mama wa watu anayeambiwa na askofu kwamba angependa kuwa naye faragha, kwa sababu “la kufanya bado sijaliona” na angependa asemezane naye na “huenda kumbe roho yako ikadunda” na piaujumbe wa kiroho unaopenyezwa bila mwenye simu kujua.
Kwa mfano, Alhajj Mourad Adul Ghafour anampigia simu mtu halafu wimbo anaousikia ni “Nibebe, Bwana Yesu, nibebe”! atajiuliza ni nini kinatokea. Au Padre Anaclet St Justus apige simu kwa ndugu yake halafu apokelewe na qasda ya sifa Mtume Muhammad (SAW), ataelewa nini?
Kampuni za simu zinafanya biashara kubwa mno nchini, na mapesa yanayovunwa na klamouni hizo wakati mwingine yanawachefua watu ambao wanadhani wanatukomoa kwa bei kali na faida za kupitiliza wanazopata, ama wale wanaoamini kwamba kampuni haya, kwa maelewano na mawakala wao serikalini,  hayalipi kodi stahiki.
Sasa wasituongezee adha na maudhi kwa kutupachikia nyimbo tusizozitaka na ambazo wakati mwingine zinaudhi hisia za kiimani. Inabidi tuiulize mamlaka ya mawasiliano, TCRA, je hili inalijua, na kama inalijua imefanya nini?
Chanzo  http://www.raiamwema.co.tz/askofu-anapokuimbia-%E2%80%9Cnataka-nipate-lau-nafas%C3%AF%E2%80%9D
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top