AMA kweli ukistaajabu wa Musa utayaona ya Firauni. Mwanamume mmoja
nchini Ghana amekiri kuwa alikubali kumuua mtoto na uanaume wake ili awe
tajiri.Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 anasema alifanya
hivyo baada ya kujiunga na kanisa moja akiwa na umri wa miaka 21 na
kupata mafundisho ya jinsi ya kupata utajiri wa haraka."Nilijiunga
na kanisa la shetani, nilimtoa sadaka mwanangu na kunywa damu yake,
nilifanya mambo mengi mabaya ambayo sikupaswa kuyafanya kama
binadamu,"anasema.
Akiwa na umri wa miaka 21, Steven Koffi (sio jina lake halisi) kutoka Accra alijiunga na kanisa hilo lijulikanalo kama Satan International.Awali, alikuwa mwanamume rijali, baba wa mtoto mmoja wa kike. Maisha yalibadilika pale alipokubali kuutoa sadaka uanaume (urijali) wake kwa sharti la kupata utajiri.Alikubaliana na masharti yote hata lile la kumtoa sadaka mtoto wake wa pekee.
Kutokana na nguvu za kiume kwisha mkewe naye alimkimbia, lakini biashara ziliendelea vizuri na kukua maradufu.Anasema sababu za kujiingiza katika kanisa hilo lilitokana na matatizo ya kifamiliana yeye kusaidiwa na rafiki yake ambaye alikutana naye katika mtandao.Rafiki huyo alimweleza habari za kanisa hilo ambalo kama atajiunga litamsaidia kifedha. Baada ya kuelekezwa alienda na kuonana na wahusika.Baada ya kuandikisha aliambiwa atakwenda Marekani kwaajili ya kukutana na mkuu wa kanisa hilo ambaye ni shetani, aliambiwa aandike barua ya kuonana na kiongozi huyo.
Anasema alifanikiwa kwenda Marekani na baada ya siku mbili alikutanishwa na shetani ambaye alimwambia aombe chochote anachohitaji."Nilimwambia shetani ninataka kuwa maarufu, tajiri na niishi miaka mingi, alinijibu anaweza kunifanikishia mawili, lakini la tatu haliwezekani kwani kila anayejiunga na kanisa hilo hufa baada ya miaka 30," anasema.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/makala/26-jungukuu/25562-aondoa-uanaume-wake-kuua-mtoto-wake-ili-atajirike

Post a Comment