Rais Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza |
Mbali na Rais Kikwete viongozi wengine
waliyoshiriki kuaga mwili wa Jaji Liundi ni Makamu wa Rais, Dk Mohammed
Gharib na Rais mstaafu Benjamini Mkapa.
Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Ofisi ya vyama vya siasa iliwakilishwa na Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya
Siasa mstaafu, John Tendwa, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja
na viongozi wa vyama vya siasa akiwamo Profesa Ibrahimu Lipumba wa
Chama Cha Wananchi CUF na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
Baada ya taratibu za kuaga mwili wa Jaji Liundi,
alizikwa jana kwenye makaburi ya Chang’ombe Maduka Mawili ambapo Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick aliongoza maziko hayo.
Post a Comment