Utata umeibuka kuhusu wabunge waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati
ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuwa wanahusika na
biashara ya pembe za ndovu.
Wakati Ofisi ya Bunge ikidai kuwa ripoti hiyo
haina majina ya wabunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli
ameshikilia kuwa majina hayo ni sehemu ya ripoti hiyo ambayo baada ya
kuwasilishwa, iliibua mjadala ambao ulisababisha mawaziri wanne
kuong’oka.
Gazeti hili limedokezwa kuwa majina ya wabunge hao
yalitajwa mbele ya kamati hiyo wakati ikichunguza jinsi Operesheni
Tokomeza Ujangili ilivyotekelezwa, baada ya kuwapo kwa malalamiko ya
vitendo vya ukatili na utesaji wa raia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge
hao hawakuitwa mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kutokana na kwamba suala
hilo halikuwa moja ya hadidu za rejea walizopewa kuzitafutia majawabu.
SOMA ZAIDI: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Majina-ya-wabunge--majangili--siri-kubwa/-/1597296/2148976/-/tl4mhpz/-/index.html
SOMA ZAIDI: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Majina-ya-wabunge--majangili--siri-kubwa/-/1597296/2148976/-/tl4mhpz/-/index.html
Post a Comment