Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka
Afrika Kusini na kuthibitishwa na Msemaji wa Hospitali ya Millpark,
Tebogo Nyembezi zinasema Dk Mvungi alifariki dunia jana mchana. “Ni
kweli tulimpokea mgonjwa huyo kutoka Tanzania na alifariki 6:00 mchana
(saa 7:00 kwa saa za Afrika Mashariki),”alisema Nyembezi.
Nyembezi alisema kwamba walimpokea mgonjwa huyo
akiwa na majeraha ya kichwa, lakini aliahidi kueleza sababu ya kifo
chake leo baada ya kuzungumza na madaktari waliokuwa wakimtibu.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba pia alithibitisha kupokea taarifa za kifo hicho na kwamba
walikuwa wakiendelea kuandaa taratibu za kuleta mwili wake nchini.
“Ni pigo kubwa kwetu, tunaangalia namna ya
kuusafirisha kuja nchini na baadaye tutatoa taarifa rasmi,”alisema Jaji
Warioba na kuongeza:
“Kwa kweli ni pigo kubwa siyo kwetu tu, lakini
pigo kubwa kwa nchi yetu, tumepoteza mtu muhimu na kiungo muhimu sana.
Dk Mvungi, wengine tulimfahamu tangu alipokuwa mwanafunzi, alikuwa mtu
aliyesema kile alichokiamini, akikwambia kitu kilikuwa ni kile kilichopo
moyoni mwake”.
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Dk-Mvungi--afariki-dunia/-/1597296/2070966/-/8ldfu2/-/index.html
Soma zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Dk-Mvungi--afariki-dunia/-/1597296/2070966/-/8ldfu2/-/index.html
Post a Comment