Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania,
Rais Jakaya Kikwete amewaaga wapiganaji wa Tanzania wanaokwenda DR Congo
kulinda amani kwa kuwadhibiti waasi wa vikundi mbalimbali kikiwamo cha
M23 walioko Mashariki wa nchi hiyo.
Kikwete alimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni
ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na Jeshi la Umoja wa Mataifa
la kulinda amani nchini humo katika hafla iliyofanyika Msangani, Kibaha,
Mkoa wa Pwani jana. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi
Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni
mwa mashuhuda katika hafla hiyo.“Ninawatakia kila la kheri kwenye mapambano,”
Amiri Jeshi Mkuu alimwambia kiongozi wa Batalioni ya Wanajeshi wa JWTZ
wanaokwenda nchini humo. Tanzania inaungana na Afrika Kusini na Malawi
kufanya kuwapo kwa kikosi cha askari 3,100 huku Tanzania ikipeleka
askari 850 kwa ajili ya kazi hiyo.
Vikosi vya awali vya Tanzania vimekwishatangulia
nchini humo vikiongozwa na Jenerali James Mwakibolwa anayeongoza Brigedi
hiyo chini ya UN, na tayari amewasili kwenye Mji wa Goma, ambao ndio
Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini unaokaliwa na waasi wa M23 tangu
Aprili 2012.Kwa mujibu wa Mtandao wa Monusco, vikosi vingine
vya wapiganaji wa Tanzania na Afrika Kusini vitawasili wiki ijayo wakati
Wanajeshi wa Malawi haijafahamika tarehe ya wao kuwasili.Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney
Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji
wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia,
kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.
Chanzo mwananchi .
Chanzo mwananchi .
Post a Comment