Kwa muda mrefu sana, nimekuwa nikiamini kuwa, Watanzania tumekuwa
tukijidanganya kudhania na kuendelea kuamini kuwa, maendeleo ya
kiteknolojia yamekuwa sababu ya kuporomoka kwa maadili ya vijana wengi
wa Kitanzania.
Na leo hii, mtazamo wangu umepata msukumo mpya baada ya kusoma kuwa,
kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia sasa, kuna Mtanzania mmoja ambaye
ataweza kujipatia kitita cha shilingi za kitanzania milioni moja
kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii. Unashangaa? Hapana,
usishangae, maana ni ukweli mtupu…… iko hivi:-
Mmoja kati ya Watanzania ambao wamejijengea heshima kubwa sana katika
jamii ndani na nje ya mipaka ya nchi, Mzee Reginald Mengi, ameahidi
kuanza kutoa kitita cha shilingi milioni moja kila mwezi kwa Mtanzania
ambaye ataandika kitu au wazo ambalo litakuwa na uelekeo wa kushinda
vita dhidi ya umasikini, kupitia ukurasa wake wa twitter.
Chanzo fuatilia : http://www.jukwaahuru.com/?p=15693
Post a Comment