Wakili Nyaga Mawalla amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa jijini Nairobi, Kenya alikokwenda kwa matibabu.Nyaga
alikufa baada ya kujirusha kutoka katika jengo la ghorofa ya hospitali
aliyokuwa akitibiwa jijini Nairobi usiku wa kuamkia juzi.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Mawalla Advocate,
John Minja aliliambia gazeti hili kuwa mwili wa marehemu ulitarajiwa
kurejeshwa nchini jana.
“Hali yake haikuwa mbaya, kwani juzi mchana
tulizungumza naye tukitaka kwenda kumsalimia lakini, alitueleza kuwa
angerejea jana nchini,”alisema Minja.Hata hivyo, bado haijajulikana sababu za kujiua, lakini baadhi ya ndugu zake wanasema ni kutokana na msongo wa mawazo.
Taarifa za kifo cha Mawalla anayemiliki
kampuni kadhaa ikiwamo Kampuni ya uwakili ya Mawalla Advocates,
kimeshtua wengi akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyesema
taifa limepoteza kijana mwenye maono, akili na mjasiriamali
aliyetajirika bila kuiba.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo
cha Nyaga. Licha ya udogo wake kiumri, lakini alikuwa mshauri wangu
kwenye mambo mengi kiuchumi, kibiashara na kijamii. Nyaga alikuwa
kiongozi wa jamii asiye na mipaka katika huduma tofauti na
wafanyabiashara wengi nchini walishirikiana naye,” alisema Mbowe.
Post a Comment