MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana 
yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, 
huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu
 na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu 
Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa
 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla
 waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na 
asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini 
waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820
 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
Fuatilia zaidi chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1698112/-/11t0745/-/index.html
  
Fuatilia zaidi chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1698112/-/11t0745/-/index.html

Post a Comment