Social Icons

Loading...

Neno La Leo: Bunge Letu Na Tuhuma Za Mke Wa Kaisari

JULIUS Kaisari  alipata kutamka; “ My wife ought not even to be under suspicion”- Kwamba mke wangu hapaswi hata kutuhumiwa.

Kaisari  alikuwa akijibu swali la kwa nini alimwacha mkewe Pompeia kwa tuhuma za kwenda kinyume na mienendo mema ya ndoa.
Ndio, tuhuma peke yake, hata kabla ya kuthibitishwa, zilitosha kwa Kaisari  kumwacha mkewe ili alinde hadhi na heshima yake. Akiamini, kuwa wenye kuhusiana na walio katika uongozi na utumishi wa umma hawapaswi kutuhumiwa kwa kutenda yalo maovu.
Hapa kwetu haijapata kutokea, kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa  kwenye tuhuma nzito ya rushwa kama ilivyo sasa. Ni vema tukatambua sasa uzito wa jambo hili; kwamba kwa Waziri mwenye dhamana  kutoa hadharani tuhuma za wabunge kuhongwa  ni kashfa kubwa. 
Si tu kwa wabunge husika, bali kwa Bunge zima, kwa Serikali nzima, kwa nchi nzima. Hakuna dawa nyingine ya kuondokana na kashfa mbaya kama hiyo isipokuwa kwa wenye kutuhumiwa kukaa pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kina na ripoti yake kwa Bunge na umma.
Maana, hapa kuna mawili yanayotarajiwa kutokea pindi ripoti ya uchunguzi itakapotoka; ama kuwatia hatiani watuhumiwa au kuwasafisha na tuhuma hizo. Hilo la kwanza likitokea ni vema na busara likaendana na hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa wahusika hata kama tayari wameshajiuzulu.

Lakini, likitokea la pili, kwamba Tume iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ikawaona watuhumiwa hawana hatia, hivyo kuwasafisha, basi, Waziri mwenye dhamana aliyetoa tuhuma hizo hadharani na watendaji wenzake wakuu wenye kuhusika na taarifa ya Waziri wanapaswa wajiuzulu mara moja. Ni kwa vile, watakuwa wamesema uongo. 
Chanzo: Raia Mwema juma hili
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top