Bunge Maalumu la Katiba limepitisha kanuni ya kuwazuia waandishi
wa habari kuingia katika vikao vya kamati za chombo hicho, hatua ambayo
inaelezwa ni kinyume na Katiba inayotoa uhuru wa wananchi kupata
habari.
Kanuni hiyo ilipitishwa jana baada ya malumbano
makali yaliyowagawa wajumbe wa bunge hilo, baadhi wakipinga kifungu
hicho kwa sababu kinavunja Katiba ya nchi inayotoa uhuru kwa waandishi
kukusanya na kusambaza habari na wengine wakiunga mkono kuwazuia.
Kanuni hiyo ilipitishwa kwa mbinde huku baadhi ya wajumbe wakiendelea
kushikilia msimamo wa kuikataa, hata baada ya Mwenyekiti wa Muda wa
bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuridhia kipite. Wajumbe waliopinga
kanuni hiyo ni Joshua Nasari, Moses Machali, Peter Serukamba, Ezekiah
Wenje na Maria Sarungi.
Baadhi ya wajumbe akiwamo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga walisimama kutaka kuzungumza lakini hawakupata fursa hiyo.
Mjumbe aliyekuwa mwiba kwa Tasnia ya Habari ni, Dk
Harrison Mwakyembe ambaye aliwashawishi wajumbe kufunga mjadala huo ili
wasonge mbele kwa madai kuwa hata yeye pia ni mwanahabari. “Hakuna
upande usiotambua umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huu...
Tunachotofautiana ni jinsi na namna
ya ushiriki wa vyombo vya habari,” alisema Dk
Mwakyembe. Alisema Taifa limeingia katika kipindi maalumu kama cha vita
na kwa msingi huo, kanuni zinabadilika kulingana na mazingira na kwamba
vyombo vya habari vinapaswa kulitambua hilo.
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Waandishi-wa-habari-wazuiwa/-/1597296/2234078/-/2npu1p/-/index.html
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Waandishi-wa-habari-wazuiwa/-/1597296/2234078/-/2npu1p/-/index.html
Post a Comment