Social Icons

Loading...

Msigwa aibana Serikali itoe majibu ripoti ya ITV London

Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, ameitaka Serikali kutoa majibu sahihi baada ya gazeti la Daily Mail on Sunday la Uingereza, kuchapisha habari inayoeleza kuwa Tanzania ni kinara wa ujangili, huku Rais Jakaya Kikwete akifumbia macho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mchungaji Msigwa alisema maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kuchapishwa kwa taarifa hizo yamejaa siasa, uzushi na uongo.
Alisema ukweli lazima uwekwe wazi kwa sababu wanaohusika na biashara hiyo ni baadhi ya watendaji wa Serikali, wafanyabiashara na vigogo wa vikosi vya ulinzi na usalama nchini.
Wakati Mchungaji Msigwa akieleza hayo, Ikulu ya Marekani jana ilitoa taarifa ya kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo ikiwa ni hatua yake ya kukabiliana na ujangili ulioshika kasi katika nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania.
Pia, leo Rais Kikwete atakuwa miongoni mwa viongozi 50 watakaohudhuria mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani, unaofanyika London, Uingereza.
Mkutano huo utakuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
Taarifa ya gazeti hilo ya Februari 8 mwaka huu, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka na kumhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na wafanyabiashara ya meno ya tembo.
Pia imewahusisha wafadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika biashara hiyo.
Katika maelezo yake Mchungaji Msigwa alisema, “Takwimu za Serikali zinaeleza wazi mwaka 2010 tembo 10,000 waliuawa nchini sawa na wastani wa tembo 37 kwa siku. Inakuwaje taarifa hizi ziwekwe wazi halafu Serikali idai inachafuliwa.”
Alisema Serikali imewahi kukiri kuwa inawajua wanaojihusisha na ujangili lakini badala ya kuwakamata imekuwa ikiwataka kuachana na biashara hiyo.
CHANZO  gazeti  la  mwananchi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top