Social Icons

Loading...

MALINZI BOSI MPYA TFF

Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.
Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni  Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
Taarifa  kwa  hisani  ya  http://www.shaffihdauda.com/

KIBONZO : NANI KAMA MAMA...


El Classico - BARCA YAIKAMUA MADRID 2-1




CHELSEA   NAO  WANG'ARA

KIBONZO- HII WADAU IMEKAAJE!!!


Blogger akutana na wadau wa UCC Arusha | Jengo la Summit Centre

 Kutoka  kushoto  ni  Stiven  Mishita, Blogger  Daudi, Blogger  Daniel, Emmanuel  Luhwavi,  na   Mr   Marcel   wadau  toka  UCC  Arusha


ACC2013 Yahitimishwa Leo AICC

Mkutano  wa  kimataifa  wa  masuala  ya  mabadiliko  ya  tabia  nchi   uliodumu  kwa  siku  nne   unakamilika  leo  hii  na   Mkrugenzi  wa  mamalaka ya   hali  ya hewa   Tanzania  Dr  Agness  Kijazi
AICC .
 Dr, Agnes  Kijazi ( koti  jekundu)  kulia  kwakae  ni  Mkurugenzi  wa  IRA  -  UDSM  Prof  Pius  Yanda  na wengine  ni  maofisa toka  WMO.
   Washindi   wakiwa  na  vyeti  walivyo   tunukiwa  na  waanadaaji  wa  ACC2013.
 Ndg  ABDALLAH  ISSA  HENKU   meneja  wa  CCC-  UDSM   akipokea  zawadi  yake    toka  kwa  maofisa  toka  WMO.
 Dr. Agness    mkurugenzi  wa  TMA   akihitimisha  mkutano.









Arusha Nyama Choma kwa WINGI.





   Wadau  wa   ACC2013  mawasiliano  wakiwa  na    mates  wa  UCC  Arusha.
     Nyama  ya  Mbuzi  ni  Tamu.



Wadau wa mawasiliano ACC2013 wakienda sawa na Conference ndani ya AICC




ACC 2013 katika Picha .

Mkutano  wa  kimataifa  wa  mabadiliko  ya  hali  ya  hewa  afrika  unaondelea  umewakutanisha    watafiti, watunga  sera na  wanasayansi  wapatao   400, toka  duniani  kote, Ulifunguliwa  na  Makamu  wa  Rais  Mhe:  Dr  Gharib   Mohamed Bilal .


 

Zitto avitikisa vyama.

Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaka kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa nchini kutokana na kutowasilisha taarifa za ukaguzi wa matumizi yake, yamevivuruga baadhi ya vyama vilivyotajwa.Vyama vya siasa vinaonekana kutoa matamshi yanayolenga kujinasua katika hoja hiyo, vikiwemo vilivyomshutumu Zitto, kuilaumu Serikali na hata vingine vimediriki kutaka ruzuku hiyo ifutwe kwa maelezo kwamba ni ubadhilifu wa fedha za umma.
Juzi Zitto alisema tangu 2009 Serikali ilitoa kiasi cha Sh67.7 bilioni kama ruzuku kwa vyama tisa vya siasa, lakini vyama hivyo havijawahi kuwasilisha taarifa za ukaguzi hesabu zake msajili kama sheria inavyoagiza. Kwa sababu hiyo, Zitto aliamuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kusimamisha utoaji wa ruzuku hadi hapo vitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi na makatibu wake wakuu kuhojiwa.
Kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya 1992 ambayo ilifanyiwa marekebisho ya Sheria namba 7 ya 2009, Vyama vya Siasa vinawajibika kuwasilisha hesabu zake kwa CAG na ofisi hiyo inaweza kuamua kuzifanyia ukaguzi yenyewe au kuteua mkaguzi.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliwahi kusema kuwa utaratibu ambao umekuwa ukitumiwa na vyama hivyo kwa kuteua kampuni binafsi siyo sahihi na ni kinyume cha sheria.“Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vinatakiwa viwasilishe hesabu kwa CAG, ndipo tuzikague au tuamue kampuni ya kufanya ukaguzi huo, sasa wao walichagua kampuni binafsi moja kwa moja zikawafanyia ukaguzi,” alisema Utouh wakati akitangaza kuthibitisha ubora wa hesabu za vyama vitano vilivyoshiriki kwenye Uchaguzu Mkuu wa 2010.
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alipendekeza kufutwa kwa ruzuku hiyo kwa vyama vya maelezo kuwa ni inawanyonya wananchi.“Badala ya kuvipa vyama vya siasa ruzuku, tuelekeze fedha hizo kwenye miradi mingine ya maendeleo,” alisema Mtikila huku akiahidi kwamba chama hicho kitawasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa taarifa yake ya fedha iliyokaguliwa katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.
chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Zitto-avitikisa-vyama/-/1597296/2035700/-/ewbfygz/-/index.html

TAARIFA TOKA TANAPA

 
 
TAARIFA KWA UMMA 
Katika Gazeti la Mawio Toleo Namba 0062 la tarehe 26.9.2013 – 02.10.2013 na toleo Namba 0063 la tarehe 03.10.2013 zimechapishwa habari zenye vichwa vya habari “Mtandao wa Ujangili Huu Hapa” na “Wabunge CCM watajwa ujangili”.
Katika habari zote hizo zimelihusisa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari hizo.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa hizi:
(i)               Shirika la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini ripoti iliyotajwa katika habari hizo kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
(ii)          Shirika husimamia shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi     
           za Taifa pekee kiutendaji, ambapo baadhi ya maeneo yaliyotajwa   
           Katika habari hizo kama Selous na Liwale kiutendaji hayapo ndani  
           ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
(iii)         Kama Shirika la Umma, hufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola katika kushughulikia uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo ujangili.
Ni kwa mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki na taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa kufanyia kazi.
Tunachukua nafasi hii kuviomba vyombo vya habari kushiriki katika juhudi za kupambana na ujangili kwa kuwa waangalifu katika kuandika habari za kutuhumiana kabla ya kuwa na ushahidi kamili ambao ni haki ya kimsingi ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.
Imetolewa na Idara ya Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
07/10/2013
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top