Social Icons

Loading...

Wakili Nyaga Kuzikwa Nairobi.

Familia ya Wakili Nyaga Mawalla imeridhia ndugu yao azikwe jijini Nairobi, Kenya na kumaliza mvutano wa suala la mazishi ya wakili huyo.Mawalla alifariki dunia jijini Nairobi baada ya kuanguka kutoka kwenye ghorofa katika hospitali alikokuwa akitibiwa Machi 23, mwaka huu.

Hata hivyo, kulizuka mvutano wa mazishi yake baada ya Wakili Fatuma Karume kupeleka wasia wa marehamu uliokuwa umeelekeza kuwa ikitokea amefia nje ya nchi azikwe huko au akifia ndani ya nchini basi azikwe kwenye shamba la Momella, Arusha wakati wazazi wake walitaka azikwe kwao Marangu mkoani Kilimanjaro.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana msemaji wa familia hiyo, Joseph Nuwamanya alisema wameamua kuheshimu wasia wa marehemu.
“Familia na ndugu wote wa mpendwa wetu Mawalla wameamua marehemu azikwe Jumatano jijini Nairobi kwani kabla ya kifo chake yeye mwenyewe alitaka azikwe sehemu atakayofia ikitokea amefia nje ya nchi,”alisema Nuwamanya. Alisema licha ya ndugu yao kuzikwa huko taarifa zaidi kuhusiana na sehemu, muda wa mazishi zitatolewa pindi utaratibu utakapokamilika.
Chanzo  : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1736640/-/129cetj/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top