Social Icons

Loading...

Rais XI JINPING ATUA NCHINI.


Rais wa China, Xi Jinping aliwasili nchini jana saa 10:5 akitumia ndege Boeng 747 ya Shirika la Ndege la China na leo atazungumza kwa mara ya kwanza na Afrika akitumia jukwaa la Tanzania.
         Jinping atatoa hotuba yake kwenye jengo jipya la kisasa la Mwalimu Nyerere ambalo limejengwa na Serikali ya China likiwa na uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa mara moja lilipo jijini.Rais huyo ambaye ameambatana na mkewe pamoja na maofisa mbalimbali wa Serikali yake,anatajiwa kutambulisha sera kwa Bara la Afrika huku wachunguzi wa mambo wakisema kuwa hotuba yake hiyo huenda itazingatia juu ya uimarisha uhusiano mwema baina ya pande zote mbili.
 China ndiyo dola inayotajwa kuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika na katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kiwango cha ufanyaji biashara baina ya pande hizo mbili kinatajwa kukua kwa asilimia 70. China pia ndiyo mshirika pekee kwa Afrika ambaye misaada yake inaambatana na masharti nafuu.
Hata hivyo ushawishi wa China barani Afrika unakosolewa na baadhi ya nchi za Magharibi zinazoituhumu China kwamba inazinyonya nchi za Afrika.
       Alipowasili jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Rais huyo alipokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na kisha alipigiwa mizinga 21 na baadaye alikagua gwaride. Baada ya mapokezi hayo ya uwanjani, Rais Jinping na mwenyeji wake walioogoza kwenda jijini ambapo jioni ya jana walikuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye walijumuika na halaika kwa ajili ya kushiriki dhifa ya taifa.
Taarifa  kwa  hisani  ya  :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1729660/-/128rxxi/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top