Social Icons

Loading...

Polisi yawaonya wanaosambaza uvumi wa Pasaka.

Msemaji wa Polisi, Advera Senso.
 Polisi imeonya kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaojihusisha na vurugu kipindi cha Sikukuu za Pasaka, zitakazoadhimishwa mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema wamekamilika na hafikirii kama kutakuwa na yeyote atakayevunja amani.

Senso alikuwa akizungunmzia kuhusu uwapo wa uvumi wa baadhi ya watu kutaka kuvuruga shughuli za ibada kuanzia Alhamisi hadi Jumatatu. “Taarifa hizo kwa kweli hatuna, wanaovumisha uchonganishi huo tunawaonya waache mara moja kwa sababu wanahatarisha amani, tukiwapata tutawachukulia hatua za kisheria,” alisema Senso.

Alisema Tanzania haina udini wala ukabila, ipo salama na ikiwa kuna mwenye ushahidi au taarifa kuhusu kusudio la uhalifu zipeleke polisi, kwani hiyo ndiyo polisi shirikishi. Kuhusu madai ya baadhi ya viongozi wa Kikristo kupeleka taarifa hizo polisi, Senso alisisitiza kuwa Tanzania haina udini na atakayevunja amani kwa namna yoyote atashughulikiwa kisheria kama mhalifu siyo kidini.

Alisema kila mwananchi anatakiwa kujilinda, kulinda mwenzake na taifa lake kwa jumla.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT), Askofu David Mwasota alilieleza Mwananchi jana kuwa, licha ya taarifa za maandishi zinazosambazwa katika simu za viganjani, wiki iliyopita Wasomali wengi walionekana wakiingia nchini na kwamba taarifu zimefikishwa polisi.

Imeandikwa na Editha Majura, Nuzulack Dausen na Pamela Chilongola
Naye Katibu wa Baraza la Maskofu Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde alikiri kuwapo taarifa za vitisho dhidi ya Wakristo katika maadhimisho ya Pasaka na kwamba, walipeleka taarifa kwenye vyombo vya usalama ili zifanyiwa kazi.
Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1730256/-/12985sq/-/index.html
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top